
SHINIKIZO            LA JUU LA DAMU: 
        Chanzo na            Tiba yake
        Nini maana ya shinikizo la juu la damu?
        Ni msukumo wa damu ulio juu kuliko inavyotakiwa kwa            muda mrefu. Msukumo wa damu huhitajika mwilini ili kusambaza            chakula, oksijeni na kutoa uchafu.
        Shinikizo la juu la damu hupimwa kwa kutumia kifaa            kinachoitwa Sphygmomanometer
        Shinikizo la juu la damu husababishwa na nini?
        Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha shinikizo la juu            la damu:
        1. Uvutaji sigara
2. Unene na uzito kupita kiasi
3. Unywaji wa pombe
4. Upungufu wa madini ya potassium
5. Upungufu wa vitamin D
6. Umri mkubwa
7. Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
8. Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin
        2. Unene na uzito kupita kiasi
3. Unywaji wa pombe
4. Upungufu wa madini ya potassium
5. Upungufu wa vitamin D
6. Umri mkubwa
7. Ongezeko la kemikali kwenye figo (renin)
8. Kushindwa kufanyakazi kwa kichocheo kiitwacho insulin
Uanishaji wa shinikizo la damu
        Presha ya kawaida <120 br="">Presha inayoelekea            kupanda 120-139 80-89
Presha hatua ya 1 140-159 90-99
Presha hatua ya 2 160-179 100-109
Presha hatua ya 3 ≥180 ≥110
        Presha hatua ya 1 140-159 90-99
Presha hatua ya 2 160-179 100-109
Presha hatua ya 3 ≥180 ≥110
Shinikizo la damu/BP ni ugonjwa unaosumbuwa watu wengi            sana duniani na hii ni kutokana na kutokujuwa ni nini hasa            husababisha ugonjwa huu mwilini. Shinikizo la damu linaonekana            kuwa ni ugonjwa wa kuishi kwa kufuata masharti.
        Katika makala hii tutaona uhusiano mkubwa uliopo kati            ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa huu, mwishoni utakuwa            umeelewa sasa ni jinsi gani ilivyo rahisi kabisa kujiepusha na            kujiponya ugonjwa huu. Endelea kusoma.
        Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema            tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na            shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo            (Heart Attacks), kupooza na kiharusi (Strokes).
        Takribani watu milioni nane hufa kila mwaka kutokana            na ugonjwa huu wa kupanda kwa shinikizo la damu.
        Dalili za shinikizo la damu:
        • Maumivu ya kichwa (Haswa nyuma ya kichwa mara nyingi            nyakati za asubuhi),
• Kuchanganyikiwa,
• Kizunguzungu,
• Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
• Kutoweza kuona vizuri au
• Matukio ya kuzirai.
• Uchovu/kujisikia kuchokachoka
• Mapigo ya moyo kwenda haraka
• Kutokuweza kuona vizuri
• Damu kutoka puani
        • Kuchanganyikiwa,
• Kizunguzungu,
• Kelele sikioni (Mvumo au Mazomeo masikioni),
• Kutoweza kuona vizuri au
• Matukio ya kuzirai.
• Uchovu/kujisikia kuchokachoka
• Mapigo ya moyo kwenda haraka
• Kutokuweza kuona vizuri
• Damu kutoka puani
Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata            vipimo.
        'Mwili wa binadamu unapopungukiwa maji hutoa ishara            (indicators), tumeziita ishara hizo kuwa ni magonjwa, hauumwi,            una kiu, usiitibu kiu na madawa – dr. Batmanghelidj'.
        Shinikizo la damu (hasa la juu) ni kiashiria cha mwili            kupungukiwa maji kwa kiwango kikubwa, ni wakati ambapo mwili            unajaribu kujizoesha na upungufu wa jumla wa maji wakati            kunapokuwa hakuna maji ya kutosha kuijaza mishipa ya damu            yenye kazi ya kusambaza maji kwenye seli mhimu.
        Mishipa ya damu imebuniwa maalumu kuendana na            mtiririko uliosawa wa ujazo wake wa damu na mahitaji            mbalimbali ya tishu kwa kufunga na kufungua mishipa mbalimbali            ya damu ndani ya mwili.
        Figo hushtuka upesi kulingana na mtiririko wa damu.            Hili linaposhindikana, yaani iwapo mtiririko au ujazo wa damu            utapungua, basi Figo huitoa homoni iitwayo 'renini' ambayo            yenyewe huzarisha kitu kiitwacho 'angiotensini' ambayo huwa na            matokeo mawili; kwanza huzibana ateri na kupandisha shinikizo            la damu, pili huisababisha tezi ya 'adreno' kutoa homoni            iitwayo 'aldosteroni' ambayo huzifanya figo kuishikilia chumvi            na hivyo kusababisha kupanda kwa shinikizo la damu.
        Asilimia 94 ya damu ni maji. Kwa ujumla kila seli            ndani ya miili yetu ina bahari ya maji baridi ndani yake na            bahari ya maji chumvi nje yake. Afya bora inategemea uwiano            mzuri wa maji ya bahari hizo mbili.
        Chumvi inayashikilia na kuyalazimisha baadhi ya maji            kubaki nje ya seli (osmotic retention) na potasiamu            inayashikilia maji ndani ya seli.
        Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji (yaani            haunywi maji ya kutosha kila siku) mwili utaongeza ujazo wa            maji chumvi kwenye bahari ya nje ya seli.
        Kupitia mfumo maalumu, homoni iitwayo 'vasopressini'            hutolewa ambayo inaweza kuyachuja maji ya chumvi toka katika            bahari ya nje ya seli na kuyachoma maji hayo baridi (baada ya            kuwa yamechujwa) ndani katikati ya bahari ya ndani ya seli            kama yanavyohitajika ili kuutunza uwiano sawa wa maji ndani na            nje ya seli.
        Lakini ili mbinu hii ifanikiwe, mbinu gani, mbinu ya            kuyachuja maji ya chumvi toka katika bahari ya nje ya seli,            vasopressini husababisha kapilari na mishipa ya damu kujikaza            au kupunguza vipenyo vyake na kukupatia wewe shinikizo la juu            la damu (BP) ambalo ni mhimu ili kuyachuja na kuyachoma maji            baridi ndani ya seli toka katika bahari ya maji chumvi iliyopo            nje ya seli.
        Kama mishipa ya damu haitapunguza vipenyo vyake,            baadhi ya gesi itaachana na damu ili kuziba nafasi zilizowazi            kutokana na kupungua kwa umajimaji mwilini na hatimaye            kukusababishia msongamano wa Gesi (Gas locks).
        Sifa hii ya vipenyo vya mishipa ya damu kujirekebisha            kwa ajili ya mzunguko wa damu, ndiyo mtindo unaotumika zaidi            katika kanuni za kihaidroliki wakati ambapo mzunguko wa damu            mwilini umejirekebisha kuendana na kiasi cha umajimaji            kinachopatikana.
        Wakati mwili unapokuwa katika upungufu wa maji kwa            mfano kutokana na kutokunywa maji ya kutosha; asilimia 66 ya            kuishiwa maji inajionesha kwa kupungua kwa ujazo wa seli,            asilimia 26 inapotea toka ujazo wa umajimaji uliopo sehemu ya            nje ya seli na asilimia 8 tu inapotea toka katika ujazo wa            damu.
        Shinikizo la juu la damu ni kiashirio cha mwili            kupungukiwa maji kwa asilimia 8 tu, lakini madhara            yanajitokeza sababu ya asilimia 66 ya kupunguwa kwa ujazo wa            seli.
        Maji na chumvi vitalirudisha shinikizo la damu katika            hali yake ya kawaida.
Hii ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza unywaji wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa bora ya kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.
        Hii ndiyo sababu shinikizo la damu linapaswa kutibiwa kwa kuongeza unywaji wa maji pekee. Dr.Batmanghelidj anasema; Maji peke yake, ni dawa bora ya kukojosha, pekee ya asili tuwezayo kuiendea.
Kama watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu            wangeongeza kiasi cha uchukuaji maji, hawatazihitaji dawa za            kukojosha, watazarisha mkojo wa kutosha na hivyo kuiondoa            chumvi iliyokuwa imezidi!. Watatakiwa pia kuacha kula vyakula            visivyo na chumvi na hivyo kuepukana na mikakamao ya mishipa            (cramps) kwenye miguu yao.
        Madhara yanayoweza kuletwa na shinikizo la damu:
        Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, kutokulielewa shinikizo            la damu kama moja ya ishara za mwili kupungukiwa maji na            kulitibu kwa dawa za kukojosha ambazo zinaukausha mwili zaidi,            baada ya muda zitasababisha;
        • Kuzibika kwa ateri za moyo na ateri ziendazo kwenye            ubongo
• Shambulio la moyo (heart attack)
• Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
• Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
• Kiharusi
• Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
• Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
        • Shambulio la moyo (heart attack)
• Mishtuko midogo midogo au mikubwa inayopelekea kuzimia
• Ugonjwa wa kibofu cha mkojo
• Kiharusi
• Kupungua kwa nguvu za kiume kwa upande wa wanaume
• Kuharibiwa kwa ubongo na matatizo ya akili kama vile kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
Daktari mwingine, Dr.David Brownstein katika kitabu            chake kiitwacho; "Salt Your Way to Live", anasema kwamba            alifundishwa katika vyuo vya kiganga kuwa chumvi husababisha            shinikizo la damu na kuwa kila mmoja lazima ale vyakula vyenye            chumvi kidogo. Na hili watu wengi wamekuwa wakiamini hivi.
        Wakati akiwatibu wagonjwa wake, anasema; alianza kuona            kuwa wale wanaotumia vyakula vyenye chumvi kidogo wanapata            matokeo ya chini au wanapata nafuu ndogo sana kutoka katika            vyakula hivyo vyenye chumvi kidogo au bila chumvi kabisa na            wengi wao walitokewa kuwa na uhaba mkubwa wa madini katika            miili yao.
        Katika utafiti wake ili kuwasaidia wagonjwa wake,            ndipo akaja na jibu la chumvi ya baharini ambayo haijasafishwa            (unrefined sea salt) ambayo huwa na madini mengine zaidi ya 80            ndani yake, alianza kuona kitu kigeni kinaanza kutokea.            Wagonjwa wake hao wakaanza kuona mashinikizo yao ya damu            yanaanza kushuka katika kiwango ambacho wanaweza kuachana            kabisa na matumizi ya dawa.
        Dr.Batmanghelidj anasema, ikiwa watu watajishughulisha            na mazoezi hasa mazoezi ya kutembea kwa miguu, watakunywa maji            halisi zaidi na kuongeza chumvi (siyo sodiamu) kidogo ya ziada            kwenye vyakula vyao, mashinikizo yao ya damu yatarudi katika            hali yake ya kawaida.
        Swali la kujiuliza; Ni zaidi ya miongo minne sasa            tangu tulipoambiwa kula vyakula vyenye chumvi kidogo ili            kuepukana na shinikizo la damu, kwanini sasa Idadi ya watu            wanaopatwa na ugonjwa huu inazidi kuongezeka?.
        Narudia tena, mwili unapoanza kuishikilia chumvi,            hufanya hivyo ili kuhifadhi maji, toka katika bahari chumvi            hiyo ya nje ya seli, maji huchujwa na kutumika wakati wa            mahitaji ya dharura.
        Maji na chumvi kwa pamoja vitalirudisha shinikizo la            damu katika hali yake ya kawaida. Kuikimbia chumvi            kunasababisha shinikizo la damu (BP) kuwa sehemu ya maisha            yetu, tutapata nafuu, lakini baada ya muda mfupi hali hurudi            ileile na pengine kuwa watumwa wa kuchagua kula hiki au kile.
        Tofauti na zamani ambapo shinikizo la juu la damu            lilipokuwa ni ugonjwa wa watu wanene au wenye uzito uliozidi            pekee, siku hizi wanene kwa wembamba, watoto kwa wakubwa            wanaugua BP.
        Mambo 11 mhimu ya kuzingatia unapokuwa na shinikizo la            juu la damu:
        1. Ongeza kiasi cha unywaji maji na chumvi kila siku
2. Kula nyama isiyo na mafuta mengi
3. Ongeza kula vyakula visivyokobolewa
4. Kula zaidi matunda, mboga za majani, karanga na maharage
5. Punguza vyakula vya viwandani vinavyoongezwa sukari nyingi
6. Punguza vyakula vyenye lehemu au kolesteroli nyingi
7. Acha kuvuta sigara na tumbaku za aina zote
8. Acha kunywa pombe
9. Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito unaopaswa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
10. Punguza mfadhaiko au stress
11. Fanya mazoezi ya viungo hasa mazoezi ya kukimbia kila siku na kama kukimbia kimbia huwezi basi kutembea kwa miguu masaa mawili kwa siku inatosha kabisa.
        2. Kula nyama isiyo na mafuta mengi
3. Ongeza kula vyakula visivyokobolewa
4. Kula zaidi matunda, mboga za majani, karanga na maharage
5. Punguza vyakula vya viwandani vinavyoongezwa sukari nyingi
6. Punguza vyakula vyenye lehemu au kolesteroli nyingi
7. Acha kuvuta sigara na tumbaku za aina zote
8. Acha kunywa pombe
9. Dhibiti uzito wako, hakikisha una uzito unaopaswa kuwa nao kwa mjibu wa urefu wako
10. Punguza mfadhaiko au stress
11. Fanya mazoezi ya viungo hasa mazoezi ya kukimbia kila siku na kama kukimbia kimbia huwezi basi kutembea kwa miguu masaa mawili kwa siku inatosha kabisa.
JUISI MCHANGANYIKO YA ASILI– Hii ni juisi nzuri sana            kwa mtu yeyote anayesumbuliwa na shinikizo la damu, vitu vingi            vinavyoingia katika juisi hii ni tiba nzuri kwa magonjwa            mengine mengi mwilini na siyo kwa shinikizo la damu peke yake.
        Hii ni juisi inayotengenezwa kutokana na mchanganyiko            wa vitu tofauti vifuatavyo:
        • Vitunguu swaumu 12
• Vitunguu maji 12
• Tangawizi 12
• Asali ya nyuki wadogo lita 1
• Ndimu 12
• Chumvi ya mawe kijiko kidogo kimoja
        • Vitunguu maji 12
• Tangawizi 12
• Asali ya nyuki wadogo lita 1
• Ndimu 12
• Chumvi ya mawe kijiko kidogo kimoja
Namna inavyoandaliwa
        1. Saga (blendi) kwa pamoja vitunguu saumu na vitunguu            maji pamoja na maji lita 2 na uchemshe kwenye moto kwa dakika            kumi. Ikipoa chuja vizuri kupata juisi yake.
        2. Saga tangawizi pamoja na maji lita 1 Ikipoa chuja            vizuri kupata juisi yake, weka pembeni kwenye bakuli safi
        3. Chukuwa limau au ndimu kata katikati kila moja na            uchemshe kwenye moto na maji lita moja kwa dakika 15.            zikishachemka subiri zipowe kisha zikamuwe na uchuje kupata            juisi yake.
        4. Changanya hizo juisi zote hapo juu katika chombo            kimoja kikubwa na kisha
        5. Ongeza asali ya nyuki wadogo mbichi nzuri lita            moja, na mwisho ongeza chumvi ya mawe kijiko kidogo cha chai            kimoja, koroga vizuri kwa pamoja.
        Ukifuata vizuri maelezo haya mwishoni utapata juisi ya            ujazo wa lita 5 au 6.
Kunywa juisi hii kikombe kimoja (robo lita) kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Juisi hii inaweza kukaa bila kuwekwa kwenye friji wiki 2 hadi 3 bila kuharibika.
        Kunywa juisi hii kikombe kimoja (robo lita) kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Juisi hii inaweza kukaa bila kuwekwa kwenye friji wiki 2 hadi 3 bila kuharibika.
Kwa            ushauri zaidi au kama unahitaji hiyo juisi mchanganyiko ya            asili, niachie ujumbe WhatsApp +1 805 855 1133
        Paul Fadhil.
        
0 comments:
Post a Comment