Moto ambao chanzo chake hakijajulikana hadi sasa umeteketeza baadhi ya mabanda ya mama lishe na mitumba karibu na kituo cha mabasi mkoani Njombe.
Hata hivyo, kikosi cha            Zimamoto mkoani humo kimefanikiwa kuuzima moto huo usiku wa            kuamkia leo ambapo polisi wamesema uchunguzi wa tukio hilo            unaendelea.
        Kwa mujibu kikosi hicho,            mabanda mengine yamesalimika katika ajali hiyo.
        Hata hivyo, kikosi hicho            kimewataka wananchi kuwa watulivu wakati huu wakisubiri            matokeo ya uchaguzi ambayo yanatarajiwa kutolewa muda wowote            mkoani humo.
        Kwa mujibu wa kituo cha            luninga cha AzamTV, polisi mkoani humo wamesema uchaguzi            mkoani humo ulifanyika kwa utulivu na hsata moto huo            ulipotokea, wananchi wengi walikuwa majumbani mwao.
        
0 comments:
Post a Comment