Na Hassan Hamad, OMKR. 
        Makamu wa Kwanza wa Rais                wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amepiga kura                katika kituo cha Garagara Shehia ya Mtoni Kidatu jimbo la                Mtopepo. Maalim Seif ambaye pia                ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi                CUF, amepiga kura katika kituo hicho mnamo majira ya saa                nne asubuhi. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada                ya kupiga kura, Maalim Seif amesema ameridhishwa na jinsi                wananchi walivyojitokeza kupiga kura, sambamba na utulivu                uliokuwepo katika kituo hicho. 
        Ameelezea matumaini yake                ya kupata ushindi katika uchaguzi huo, na kwamba iwapo                uchaguzi utafanyika katika hali ya uhuru, haki na uwazi                atakubaliana na matokeo ya uchaguzi huo. 
        ![]()  |             
| Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasili katika kituo cha kupigia kura cha Garagara kwa ajili ya kupiga kura. | 
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa                  Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhiwa                  karatasi za kupigia kura tayari kwa kwenda kupiga kura
                   Makamu wa Kwanza wa Rais wa                  Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitumbukiza                  karatasi ya kupigia kura kwenye sanduku la kura.
        Makamu wa                Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,                akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura                katika kituo cha Garagara jimbo la Mtopepo. Picha na OMKR
        



0 comments:
Post a Comment