October 14, 2015

  • THOMAS SANKARA ALIUAWA KINYAMA


    THOMAS SANKARA ALIUAWA KINYAMA
    Image copyrightAFP
    Image captionThomas Sankara
    Matokeo ya ukaguzi wa kimatibabu uliofanyiwa mabaki ya mwili wa aliyekuwa rais wa Burkina Faso marehemu Thomas Sankara miaka 28 baada ya kuuawa,yanaonyesha kuwa mwili wake ulijaa risasi kulingana na wakili aliyekuwa akiwakilisha familia yake kulingana na mtandao wa facebook wa kituo cha habari cha Burkina 24.


    Familia yake ilikuwa ikingojea matokeo ya DNA kuthibitisha kwamba mabaki hayo yalikuwa ya bwana Sankara,wakili Benewende Sankara aliviambia vyombo vya habari nchini humo.
    Image copyright
    Image captionMariam Sankara mkewe marehemu Thomas Sankara
    Bwana Sankara aliuawa katika mazingira ya kutatanisha akiwa na umri wa miaka 37 na kundi la wanajeshi mwezi Octoba mwaka 1987,na alizikwa kwaa haraka kufuatia mpainduzi yalioongozwa na mrithi wake Blaise Compaore
    BBC.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.