Mgombea urais kupitia              chama cha Chadema anayeungwa mkono na vyama vinne              vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa              amesema watanzania wakimpa ridhaa ya kuongoza nchi              atahakikisha anadhibiti vifo vya mama na mtoto.
            
            
            
                                                                             
        Majira ya saa nane mchana                akiwa kwenye jukwaa la kampeni mjini Moshi.
            Sauti ileile pia                ilisikika majira ya saa tano asubihi alipowasili Tarakea                mjini Rombo.
            Edwrad Lowassa anayetamba                kama mkombozi wa Tanzania ijayo, amesema kama watanzania                watampa ridhaa ya kuwa rais atahakikisha anadhibiti vifo                vya mama na mtoto hapa nchini.
            Akiwa mjini Tarakea                mpakani mwa Tanzania na Kenya akatumia jukwaa hilo                kutangaza neema kwa watanzania waishio mipakani
            Freeman Mbowe mwenyekiti                wa Chadema taifa anasema nafasi hii ni muhimu kwa                watanzania kuitumia kwa kukiondosha madarakani chama cha                CCM kwani licha ya kushindwa kuleta mabadiliko bali pia                kimechoka na hakipaswi kuendelea kuwepo madarkani.
            Akiwa mjini Kilimanjaro                Edwrad Lowassa usafiri wa chopa ulimrahisishia kazi kwa                kufanya mikutano katika majimbo ya Rombo, Moshi mjini,                Siha na Karatu ambapo comledy Kingunge Ng'ombale Mwiru                akatoa neno kwa watanzania. 
          
0 comments:
Post a Comment