October 13, 2015

  • ALIYEDHANIWA AMEFARIKI AAMKA KABLA YA UPASUAJI

    HospitaliImage copyrightSPLImage captionMadaktari wanasema mwanamume huyo alipimwa mpigo wa moyo na damu kabla ya kufanywa kwa uamuzi kwamba alikuwa amefariki
    Wahudumu katika chumba cha kuhifadhia maiti mjini Mumbai walipigwa na butwaa baada ya mwanamume kuamka muda mfupi kabla ya kufanyiwa upasuaji.


    Daktari mkuu alikuwa amesema mwanamume huyo wa miaka 50 alikuwa amefariki na akaagiza mwili wake upelekwe mochari mara moja.
    Agizo hilo lilikiuka kanuni za hospitali kwani watu wanaotangazwa kufariki hutakiwa kukaa kwenye wadi saa mbili, kuhakikisha hakuna kosa na ni kweli wamefariki dunia.
    Madaktari wanasema mwanamume huyo kwa jina Prakash alikuwa na matatizo ya mwili kuendesha shughuli za kawaida na alikuwa akiropokwa alipofikishwa hospitalini.
    Vyombo vya habari nchini humo vinasema alipatikana katika kituo cha mabasi akiwa amepoteza fahamu.
    Akiongea katika kikao cha wanahabari Jumatatu, Dkt Suleman Merchant, anayesimamia hospitali ya Lokmanya Tilak alisema Prakash ni mlevi "aliyejitelekeza" na alikuwa na mabuu usoni na masikioni.
    "Miili ya wafu kawaida ndiyo huwa na mabuu. Lazima alikuwa amekaa pahali amelala siku sita au saba," alisema daktari Merchant.
    Aliambia wanahabari kwamba daktari aliyemchunguza Prakash alimpima mpigo wa moyo, mpigo wa damu na hata kupumua kwake.
    Dkt Merchant amesema hospitali hiyo imeanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.
    Prakash yuko katika hali thabiti hospitalini ambako anaendelea kutibiwa.
    BBC.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.