Msanii wa Bongo Joseph Haule maarufu kwa jina 'Profesa            Jay' ndiye msanii wa hivi karibuni kuwahi kushinda kiti cha            ubunge nchini Tanzania.
        Msanii huyo wa muziki wa Rap alitangazwa mshindi wa            kiti cha eneo bunge la Mikumi katika uchaguzi huo baada ya            kupata kura 32,259.
        Profesa Jay ambaye alikuwa akiwania kiti hicho kwa            tiketi ya chama cha CHADEMA alimshinda mpinzani wake wa Chama            cha mapinduzi CCM, Jonas Nkya ambaye alijipatika kura 30,425.
        Msanii huyo ni wa pili sasa kuchaguliwa baada ya            meneja wa bendi ya Yamoto Said Fella kuchaguliwa kama diwani            wa wadi ya Kilungule jimbo la Mbagala.
        
0 comments:
Post a Comment