Rais              Dk.Jakaya Kikwete akizungumza leo wananchi wa Bagamoyo              katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Bandari              ya Bagamoyo.
                Rais              Dk.Jakaya Kikwete akifungua pazia kwa kuweka jiwe la msingi              la uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo leo.
                Waziri              Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza leo wananchi wa Bagamoyo              katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa Bandari              ya Bagamoyo.
        Waziri              wa Uchukuzi,Samwel Sitta akizungumza leo wananchi wa              Bagamoyo juu ya ujenzi wa bandari ya Bangamoyo. 
                Makamu              wa Rais Mtendaji wa Umoja wa Wafanyabiashara wa China, Dk.Hu              Jianhua akizungumza katika uzinduzi wa Bandari ya Bagamoyo              leo. 
                Sehemu              ya viongozi wa waliohudhuria uwekaji wa jiwe la la msingi na              uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo leo.
                Rais              Jakaya Kikwete akiwa katika picha na viongozi mbalimbali              baada ya kuweka jiwe la msingi na ujenzi wa bandari ya              bagamoyo leo.
                Baadhi              ya wananchi wa Bagamoyo waliohudhuria uwekaji wa jiwe la              msingi la ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.Na              Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
        RAIS              DK.Jakaya Kikwete ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo              kufanya tathimini upya kwa wakazi wa vijiji vitatu              wanaopisha bandari ya Bagamoyo.
        Dk.Kikwete              ameyasema hayo leo Bagamoyo wakati wa kuweka jiwe la msingi              la uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ,amesema kuwa              wananchi wasiondoke katika maeneo yao wakiwa na manunguniko.
        Amesema              kuwa mradi wa ujenzi ni mkubwa hivyo wananchi wanatakiwa              kupewa haki yake kutokana na eneo ikiwa pamoja na kujengewa              nyumba katika kuanza upya kwa makazi ya Kidagoni.
        Rais              Kikwete amesema mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo              umekuja wakati mwafaka kwa kuongeza fursa nyingi baada ya              kukamilika kwa mradi huo na kuongeza uchumi wa nchi.
        Aidha              ameiagiza Mthamini wa Halmashauri kutafutiwa sehemu nyingine              kutokana na kufanya tathimini isiyoendana na malipo hali ya              wakazi hao ambao wameachia eneo hilo kwa ajili ya uchumi.
        "Nchi              haiwezi kuwa safi kuwepo mradi mkubwa wa bandari kubwa              Afrika lakini wananchi waliocha eneo hilo wakiwa              wananungunika kwa kupuchwa mali zao kwa ajili ya mtu mmoja              tu"amesema Rais Jakaya. 
        (              Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya Jamii)
        
0 comments:
Post a Comment