Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar          kimesema hakina imani na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika          uendeshaji nzima wa uchaguzi. 
        Akizungumza na waandishi wa          habari visiwani hapa Naibu katibu mkuu CCM Bwana Vua Ali Vuai          amesema baadhi ya maeneo mawakala wa Chama chao walinyimwa          vitamulisho jambo ambalo limekifanya chama hicho kutokuridhika          na utaratibu huo. 
        Amesema siku moja kabla ya          uchaguzi walifika tume ya uchaguzi kuhakiki vitambulisho vya          mawakala wao wote na vilikuwepo. 
        Amesema cha kushangaza ni kuwa          siku ya kura vitambulisho vya mawakala hao havikuonekana wala          hakujulikana nani alivichukua
        "Kutokana na hali hii tunakosa          imani na ZEC " alisema Vuai.
        ANGALIA VIDEO HAPA: 
0 comments:
Post a Comment