Mwenyekiti wa Chadema, mh Freeman Mbowe amemtaka Rais Kikwete kutovuruga amani ya nchi na badala yake amemtaka aondoke madarakani na kuiacha nchi ikiwa salama.
Alisema                Rais Kikwete  anatakiwa aondoke madarakani salama kama                walivyofanya marais wenzake wastaafu.
                "Rais                  Kikwete ameamua kuwa mpiga debe wa Magufuli (mgombea wa                  CCM), sasa mimi naomba nimjibu yeye kama mpiga debe na                  si rais," alisema Mbowe.
                Alisema                Rais Kikwete ameamua kuwaaminisha  Watanzania kuwa wapiga                kura wapo milioni 28 badala ya milioni 22 kama                ilivyotangazwa na Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi                (Nec).
                "Sasa                  nataka kumuuliza Rais Kikwete hao wapiga kura wengine                  milioni sita wametoka wapi?" alihoji Mbowe na                kuongeza:
                "Naomba                  kumwambia Rais Kikwete kuwa hii nchi si yake, hii nchi                  si ya CCM na hii nchi si ya familia yake...hii ni nchi                  ya Watanzania," alisema.
                Alisema                hatua ya Rais Kikwete na CCM inayoungwa mkono na Nec                kuwataka wananchi wapige kura na kuondoka vituoni                haiwatendei haki Watanzania.
                "Kikatiba                  Watanzania wana haki ya kulinda kura zao kwa sababu zile                  ni kura zao, nashangaa Rais Kikwete anawaambia watu                  waondoke," alisema.
                Mbowe,                aliwaomba Watanzania wote kwenda kwenye vituo kwa ajili ya                kupiga kura ikiwa ni pamoja na kuzilinda kura zao.
                Pia                alisema anashangazwa na kauli ya Rais Kikwete ya kuliagiza                Jeshi la Polisi kuwaondoa wananchi kwa nguvu katika vituo                vya kupigia kura.
                "Hao                  askari walioagizwa na Rais Kikwete, nao wana watoto na                  familia zao, naomba nikwambie Rais Kikwete kuwa huwezi                  kuzuia mabadiliko. Zimebaki siku 11, Mungu atajibu                  maombi yetu...nawaambia wananchi nendeni mkapige kura                  kaeni mita 200 lindeni kura zetu," alisema.
Akiwa mjini Dodoma jana wakati wa kilele cha Mwenge wa Uhuru kilichoenda sanjari na kumbukumbu ya miaka 16 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais Kikwete alitaja idadi kubwa ya wapiga kura kuliko iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Hata hivyo, jana jioni Ikulu ililitolea ufafanuzi suala hilo na kudai kuwa idadi kamili ya wapiga kura ni milioni 22 na si vinginevyo.
"..... Katika Kilele cha mbio za mwenge wa uhuru , kumbukumbu ya Baba wa Taifa , Mwalimu JULIUS Nyerere na wiki ya vijana Kitaifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hotuba yake amezungumzia idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura.
"Kwa uhakika amesema kuwa idadi ya wapiga kura ni 22,751, 292 kwa upande wa Bara na 503,193 wa Zanzibar. Hii ndiyo idadi kamili ambayo imo kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais na hii ndiyo idadi kamili kama ilivyotolewa na Tume ya Uchaguzi Tanzania.." Ilisema Sehemu ya Tamko hilo la Ikulu jana.

0 comments:
Post a Comment