Mwanasheria Mkuu wa Serikali,              George Masaju ametoa mwongozo wa kisheria kufuatia              sintofahamu iliyoibuka kwa baadhi ya watanzania kuhusu              sababu zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu              kutovunjwa kwa baraza la mawaziri hadi muda huu huku zikiwa              zimebaki siku tano kufanya uchaguzi mkuu. 
        Masaju alieleza kuwa kisheria              bado sio muda muafaka wa kuvunja baraza la mawaziri kwa kuwa              waziri hupoteza sifa za kuwa waziri wa serikali ya Tanzania              punde kabla ya rais mpya kupatikana. 
        "Mara tu kabla rais mteule              hajashika madaraka hayo, ndipo waziri anapoteza nafasi yake              ya kuwa waziri. Kwahiyo sasa hata uchaguzi hatujafanya,"              alisema.
                Aliongeza kuwa suala la siku              chache zilizobaki bado liko kisheria kwa kuwa rais mpya bado              hajapatikana. 
        "Japokuwa ni siku tano sasa              zimebaki, lakini uchaguzi ukishafanyika na rais akapatikana,              mara tu huyu rais mteule hajashika madaraka hayo ndipo              waziri anapoteza sifa ya kuwa waziri," aliongeza.
        Majibu ya kisheria ya mwanasheria              mkuu wa serikali yamekuja wakati ambapo taarifa zilizosambaa              kwenye mitandao ya kijamii na vijiweni zikieleza kuwa huenda              kutovunjwa kwa baraza la mawaziri kunacheleweshwa kwakuwa              kuna hofu ya mawaziri wengi kukihama Chama Cha Mapinduzi. 
        Balozi Juma Mwapachu alikoleza              tetesi hizo wakati alipokuwa akirudisha kadi ya Chama Cha              Mapinduzi katika ofisi za chama hicho zilizoko Mikocheni,              Dar es Salaam baada ya kueleza kuwa uamuzi wake unaungwa              mkono na mawaziri wengi wa serikali ya awamu ya nne.
        
0 comments:
Post a Comment