Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

October 31, 2015

  • MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015


    MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2015















































  • October 29, 2015

  • Marekani Yalaani Kufutwa kwa Matokeo Ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar


    Marekani Yalaani Kufutwa kwa Matokeo Ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar

    Marekani imelaani hatua ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC ya kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais pamoja na wajumbe wa bunge la wawakilishi visiwani humo.

    Katika taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa ubalozi huo nchini Tanzania, Marekani ilisema imeshtushwa na hatua hiyo na kutoa wito tume hiyo iondoe tamko hilo.

    Zec imeahidi kutangaza tarehe mpya ya marudio ya uchaguzi huo.

    Katika kufutilia mbali matokeo ya urais wa Zanzibar, tume ya uchaguzi ya Zanzibar-ZEC ilisema shughuli nzima ya upigaji kura visiwani iligubikwa na kasoro nyingi.

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha alisema baadhi ya makamishna wa tume hiyo, badala ya kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa kikatiba "wamekuwa ni wawakilishi wa vyama vyao".

    "Kumegundulika kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa baadhi ya vituo hasa Pemba vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura wa kituo husika."

    Alisema hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba "baadhi ya wapiga kura hawakwenda kuchukua vitambulisho vyao vya kupigia kura".

    Kadhalika, alisema kura hazikupata ulinzi mzuri hususan kisiwani Pemba ambako alisema kuwa baadhi ya mawakala wa baadhi ya vya vyama vya siasa katika kisiwa hicho walifukuzwa.

    Hata hivyo, taarifa ya ubalozi wa Marekani inasema kufutilia mbali matokeo hayo kunasitisha mchakato wa uchaguzi uliofanyika vizuri na kwa amani.

    Aidha Taarifa hiyo inasema kuwa hatua hiyo ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar inakwenda kinyume kabisa na tathmini ya waangalizi wa uchaguzi kutoka ubalozi wa Marekani, jumuiya ya ulaya, jumuiya ya madola na jumui ya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki.


  • Makamishna wapinga kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar



    Makamishna wapinga kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar   . Muda mchache baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim, kutangaza jaribio lake la kuufuta uchaguzi mkuu wa2015, makamishna wawili wa Tume hiyo, Ayoub Bakar na Nassor Khamis, wameuita uamuzi huo kuwa "si wa ZEC, bali wa Jecha binafsi" na wamejitenga mbali nao. Endelea kuambatana nasi.

  • APIGWA KWA KUZANIWA MWIZI


    APIGWA KWA KUZANIWA MWIZI


    SWADAKTA! Katika hali ya kustaajabisha, kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhan, ambaye mwishoni mwa wiki amejikuta akishushiwa kipigo kwa kudhaniwa kuwa kibaka, alisalimika baada ya kuanza kusali kwa kuwashtakia kwa Mwenyezi Mungu waliokuwa wakimpiga, akisema hakuwa na hatia na ghafla watu hao kusitisha kipigo.

    Ramadhan alikutana na hali hiyo baada ya kutuhumiwa kuiba redio kutoka katika duka moja lililopo stendi ya daladala mjini hapa.

    Ilidaiwa kuwa kibaka huyo baada ya kuchukua redio hiyo alianza kukimbia kutokana na mwenye duka kumwitia mwizi na Ramadhan akawa mmoja kati ya watu waliokuwa wakimfukuza, kabla ya mdokozi huyo kujichanganya na watu hivyo kutotambulika kirahisi.

    Baada ya kuona hivyo, wananchi hao wenye hasira walimgeukia kijana huyo na kuanza kumpa kipigo kama cha mbwa mwizi kwa vile nguo zake zilikuwa zimefanana na zile zilizokuwa zimevaliwa na kibaka aliyekuwa akifukuzwa.

    "Ewe Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, kwa msaada wako niepushie na mtihani huu niliosingiziwa kwani wewe ndiwe unayejua ukweli wa tukio hili," mtu huyo alisikika akisema kufuatia kipigo alichokuwa akikipata, baada ya kukimbia na kwenda kujibanza pembeni ya duka linalouza vinywaji baridi.

    Kufuatia maneno hayo, watu wote walijikuta wakisitisha zoezi la kumpiga na mmoja wa bodaboda wa kijiwe cha Juwata aliingia kati na kusema; "Jamani huyu jamaa anaonekana siyo mwizi na ni mtu wa dini, hivyo naomba aliyeibiwa ajitokeze na kutoa ushuhuda," alisema na hakuna aliyejitokeza.

    Kijana Ramadhan akishusha dua zito baada ya kushushiwa kipigo kikali.
    Baada ya kuona hivyo, kijana huyo aliwataka watu hao kumuacha aende zake huku baadhi ya walioshiriki kumpiga wakimuomba msamaha mtu huyo aliyekuwa akivuja damu mwili mzima.Akizungumza na mwandishi wetu, Ramadhan alisema alishuka kwenye daladala na kuungana na watu waliokuwa wakimfukuza mwizi kabla hawajamgeuzia kibao kutokana na nguo zake kufanana na za kibaka.

    "Mwizi alijichanganya na watu ndipo nikageukiwa mimi, nikakimbilia hapa dukani kwa Mhindi na kuamua kuomba msaada kwa Mungu kwa kuomba na akafanikiwa kuniokoa," alisema kijana huyo.

    Katika stendi ya daladala, mfanyabiashara wa duka lililoibiwa, aliyejitambulisha kwa jina la Shaaban, alisema alikuwa amekwenda kutafuta chenchi, ndipo alipomuona mtu akiondoka na redio yake na yeye akapiga kelele za mwizi, akadondosha bidhaa hiyo na kukimbia, lakini akashindwa kuungana na watu kumkimbiza kwa vile hakukuwa na mtu mwingine dukani.

    Wananchi wenye hasira kali wakiwa eneo la tukio.


  • SUDAN KUSINI WALIBAKA NA KULA WATU-AU


    SUDAN KUSINI WALIBAKA NA KULA WATU-AU
    Image copyrightAFP
    Image captionRipoti hiyo imeorodhesha matukio ya utekaji na udhalilishwaji wa wanawake.
    Muungano wa Afrika umeilaumu jeshi la serikali ya Sudan Kusini na vikosi vya waasi kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita.


    Uchunguzi wa AU ulibaini kuwa mapigano yaliyotokea mwezi Disemba mwaka 2013 yalitokana na mzozo kati ya makabila ya Dinka na Nuer ndani ya kikosi cha kumlinda rais.
    Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa vikosi hivyo hasimu viliwachinja watu na kuwalazimisha watu waliodhaniwa kuwa mahasimu wao kula nyama ya binadamu na kunywa damu yao.
    Image copyrightbbc
    Image captionUchunguzi huo umebaini kuwa vikosi hivyo hasimu viliwachinja watu na kuwalazimisha watu waliodhaniwa kuwa mahasimu wao kula nyama ya binadamu na kunywa damu yao.
    Jopo hilo la uchunguzi chini ya aliyekuwa rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo limepata majina ya watu wanaodhaniwa kuwa walioendesha kampeini hizo za ubakaji wa wanawake na ulaji wa watu.
    Ripoti hiyo imeorodhesha matukio ya utekaji na udhalilishwaji wa wanawake.
    Aidha majina ya watu waliotekeleza matukio hayo imebainika kuwa ni ya raia ambao hawakuwa wakishiriki vita vyenyewe.
    Image copyrightBBC World Service
    Image captionMatukio mabaya zaidi yaliripotiwa katika miji ya Juba, Bor, Bentiu na Malakal.
    Matukio mabaya zaidi yaliripotiwa katika miji ya Juba, Bor, Bentiu na Malakal.
    Watu kadhaa walioshuhudia mwanzo wa vita hivyo mjini Juba wanasema kuwa walilazimishwa kunywa damu ya watu ambao ndio walikuwa wameuawa.
    Makaburi ya halaiki pia yalifichuliwa katika uchunguzi huo ulioendeshwa tangu mwaka jana jopo hilo la uchunguzi lilipoundwa.
    Image copyrightReuters
    Image captionMakubaliano baina ya viongozi wakuu yamekiukwa
    Jopo hilo limependekeza watu waliotajwa wafikishwe katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyoundwa na muungano huo wa Afrika.
    Licha ya hofu ya kuwa maelfu ya watu wa kabila fulani walilengwa na kuuawa jopo hilo linasema kuwa Hakukuwa na ushahidi uliopatikana wa kuthibitisha kuwa kulifanyika mauaji ya kimbari.
    Image captionMiji ya Juba, Bor, Bentiu na Malakal ndio iliyoathirika zaidi
    Maelfu ya watu wameripotiwa kufariki tangu kuanza kwa vita hivyo yapata miaka miwili.
    Watu zaidi ya milioni mbili wamelazimika kutoroka makwao na kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani.


  • October 28, 2015

  • Profesa Jay ashinda kiti cha ubunge TZ


    Profesa Jay ashinda kiti cha ubunge TZ
    Image captionProfesa jay
    Msanii wa Bongo Joseph Haule maarufu kwa jina 'Profesa Jay' ndiye msanii wa hivi karibuni kuwahi kushinda kiti cha ubunge nchini Tanzania.


    Msanii huyo wa muziki wa Rap alitangazwa mshindi wa kiti cha eneo bunge la Mikumi katika uchaguzi huo baada ya kupata kura 32,259.
    Profesa Jay ambaye alikuwa akiwania kiti hicho kwa tiketi ya chama cha CHADEMA alimshinda mpinzani wake wa Chama cha mapinduzi CCM, Jonas Nkya ambaye alijipatika kura 30,425.
    Msanii huyo ni wa pili sasa kuchaguliwa baada ya meneja wa bendi ya Yamoto Said Fella kuchaguliwa kama diwani wa wadi ya Kilungule jimbo la Mbagala.


  • October 27, 2015

  • CCM Wailalamikia tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)



    CCM Wailalamikia tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)
    Na Mhamed khamis Zanzibar. 

    Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar kimesema hakina imani na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika uendeshaji nzima wa uchaguzi. 

    Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa Naibu katibu mkuu CCM Bwana Vua Ali Vuai amesema baadhi ya maeneo mawakala wa Chama chao walinyimwa vitamulisho jambo ambalo limekifanya chama hicho kutokuridhika na utaratibu huo. 

    Amesema siku moja kabla ya uchaguzi walifika tume ya uchaguzi kuhakiki vitambulisho vya mawakala wao wote na vilikuwepo. 

    Amesema cha kushangaza ni kuwa siku ya kura vitambulisho vya mawakala hao havikuonekana wala hakujulikana nani alivichukua

    "Kutokana na hali hii tunakosa imani na ZEC " alisema Vuai.
    ANGALIA VIDEO HAPA:


  • October 26, 2015

  • NEWS UPDATE: Mabomu ya Machozi Yarindima Mwanza Kuwatawanya Wafuasi wa Chadema Walioingia Barabarani Kushangilia Ushindi


    NEWS UPDATE: Mabomu ya Machozi Yarindima Mwanza Kuwatawanya Wafuasi wa Chadema Walioingia Barabarani Kushangilia Ushindi

    Polisi mkoani Mwanza jana walitumia mabomu ya machozi  kuwatawanya watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chadema  walioingia mitaani kushangilia wakiamini wagombea wao wanaongoza katika matokeo ya awali.

    Tukio hilo lilitokea kwenye kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Mlimani, eneo la Butimba, Ghana na Shule ya Msingi Buzuluga kwenye majimbo ya Nyamagana na Ilemela.

    Taarifa toka jijini Mwanza zinasema kundi la watu waliokuwa vituoni wakisubiri kubandikwa kwa matokeo hayo, lililipuka kwa shangwe, nderemo na shamrashamra baada ya matokeo hayo kubandikwa na wasimamizi wa uchaguzi wakiamini wagombea wao wanaongoza.

    Baafa  ya  hali  hiyo, polisi waliingilia kati na kufyatua mabomu ya machozi kutawanya wafuasi hao.

    Katika uchaguzi wa mwaka huu, mgombea ubunge wa Chadema na mbunge anayemaliza muda wake katika jimbo la Nyamagana, Ezekiel Wenje anachuana vikali na aliyekuwa Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula wa CCM.

    Katika jimbo la Ilemela, mbunge anayemaliza muda wake, Highness Kiwia wa Chadema anatetea nafasi yake kwa kupambana na mgombea wa CCM, Anjela Mabula.

    Uchaguzi wa urais, ubunge na udiwani umefanyika jana Oktoba 25, mwaka huu ambapo takribani Watanzania milioni 22.7 wamejiandikisha kwenye daftari la kudumu kwa upande wa Tanzania Bara huku kwa upande wa Zanzibar zaidi ya wapigakura laki tano wamejiandikisha.


  • Vibanda vya Mama Lishe na Mitumba Vyachomwa Moto Mkoani Njombe....Polisi Yawataka Wananchi Kuwa Watulivu Wakati Wakisubiri Matokeo



    Vibanda vya Mama Lishe na Mitumba Vyachomwa Moto Mkoani Njombe....Polisi Yawataka Wananchi Kuwa Watulivu Wakati Wakisubiri Matokeo

    Moto ambao chanzo chake hakijajulikana hadi sasa umeteketeza baadhi ya mabanda ya mama lishe na mitumba karibu na kituo cha mabasi mkoani Njombe.

    Hata hivyo, kikosi cha Zimamoto mkoani humo kimefanikiwa kuuzima moto huo usiku wa kuamkia leo ambapo polisi wamesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

    Kwa mujibu kikosi hicho, mabanda mengine yamesalimika katika ajali hiyo.

    Hata hivyo, kikosi hicho kimewataka wananchi kuwa watulivu wakati huu wakisubiri matokeo ya uchaguzi ambayo yanatarajiwa kutolewa muda wowote mkoani humo.

    Kwa mujibu wa kituo cha luninga cha AzamTV, polisi mkoani humo wamesema uchaguzi mkoani humo ulifanyika kwa utulivu na hsata moto huo ulipotokea, wananchi wengi walikuwa majumbani mwao.


  • October 25, 2015

  • MAALIM SEIF APIGA KURA KITUO CHA GARAGARA MTONI KIDATU UNGUJA



    MAALIM SEIF APIGA KURA KITUO CHA GARAGARA MTONI KIDATU UNGUJA
    Na Hassan Hamad, OMKR. 
    Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amepiga kura katika kituo cha Garagara Shehia ya Mtoni Kidatu jimbo la Mtopepo. Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF, amepiga kura katika kituo hicho mnamo majira ya saa nne asubuhi. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura, Maalim Seif amesema ameridhishwa na jinsi wananchi walivyojitokeza kupiga kura, sambamba na utulivu uliokuwepo katika kituo hicho. 
    Ameelezea matumaini yake ya kupata ushindi katika uchaguzi huo, na kwamba iwapo uchaguzi utafanyika katika hali ya uhuru, haki na uwazi atakubaliana na matokeo ya uchaguzi huo.
    Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasili katika kituo cha kupigia kura cha Garagara kwa ajili ya kupiga kura.
     Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhiwa karatasi za kupigia kura tayari kwa kwenda kupiga kura
       Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitumbukiza karatasi ya kupigia kura kwenye sanduku la kura.

    Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika kituo cha Garagara jimbo la Mtopepo. Picha na OMKR


  • Video..Kura fake zaokotwa Bukoba shule ya sekondari Kahororo zikiwa zimeshatikiwa .



    Video..Kura fake zaokotwa Bukoba shule ya sekondari Kahororo zikiwa zimeshatikiwa .
    Kupitia ITV imeripotiwa huko BUKOBA vijijini hali  baada ya wanafunzi wa shule ya secondari KAHORORO kupewa  shahada ya kupigiakura Ili wazidumbukize katika masanduku ya kura Richa ya kwamba hawakuwa wapiga kura wa eneo hilo.

    Shahada hizo ambazo kama unavyoona kutoka kwenye Video ya Taarifa ya Habari zikiwa zime tikiwa .

    AngaliaVideo hapo chini..




  • Uchaguzi Wahairishwa Bariadi Kwa Kukosa Karatasi za Udiwani



    Uchaguzi Wahairishwa Bariadi Kwa Kukosa Karatasi za Udiwani

    Wakati zoezi la upigaji kura likiendelea nchi nzima wakazi wa kata ya Matongo, jimbo la Bariadi, mkoani Simiyu wameshindwa kupiga kura  kwa nafasi ya udiwani   kwa kile kinachodaiwa uhaba wa karatasi za kupigia kura.

     Akiongea na waandishi wa habari Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo Abdallah Malela amesema kukosekana kwa karatasi ndicho chanzo cha uchaguzi kwa ngazi ya udiwani kusitishwa katika eneo hilo.

     Alisema kuwa kata hiyo ina jumla ya wapiga kura 7500, na vituo 17 lakini karatasi ambazo zimetoka Tume ya uchaguzi zilikuwa 3400 tu, huku zaidi ya wapigakura 4100 wakikosa karatasi hizo za kupigia kura.

    "Baada ya kuona hali hiyo niliwasiliana na viongozi wa tume kutoa taarifa ambao waliamua kuhairisha zoezi kwa nafasi ya udiwani tu, mpaka tena itakapotangazwa na tume," alsiema Malela.

     Kwa upande wa rais  na mbunge, zoezi liliendelea kama kawaida kwa kuwa karatasi hizo zililetwa za kutosha.

     Kwa upande wa Jimbo la  Itilima  Mkoani hapa  Msimamizi wa uchaguzi Alphonce Aloyce alisema zoezi lilienda salama licha ya mihuri kukwama ingawa tatizo hilo lilipatiwa ufumbuzi mapema.


  • WAKAZI WA JIJI LA MBEYA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA, MADUKA YAFUNGWA KUAJILI YA UCHAGUZI




    WAKAZI WA JIJI LA MBEYA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA, MADUKA YAFUNGWA KUAJILI YA UCHAGUZI

    Wakazi wa Jiji la Mbeya Mjini wajitokeza kwa wingi kupiga kura katika Vituo mbalimbali walivyo jiandikishia kuajili ya kupiga Kura kama waonekanavyo hapo katika Picha ni baadhi ya watu wakiwa katika kituo kilichopo Mtaa wa Mkombozi Jijini Mbeya wakiwa wamepanga Foleni kuajili ya kupiga Kura.

    Baadhi ya Wapiga kura wakiwa katika Foleni..

    Hapa ni eneo la Mwanjelwa maharufu kwa Jina la Mtaa wa kongo likiwa Pweke kuajili ya uchaguzi hakuna alie leta Biashara yake hapa siku hii ya leo..

    Baadhii ya Maduka ya Vitu vya Jumla na Lejaleja yakiwa yamefungwa Eneo la Kabwa Stendi..

    Jeshi la Polisi linaendelea kuzungukia Mitaa mbalimbali kuhakikisha hali ya Usalama  jijini mbeya Inakuwa shwari katika kipindi hiki cha uchaguzi.


  • Mgombea urais wa TLP, Macmillan Lyimo amepiga kura yake muda mfupi uliopita



    Mgombea urais wa TLP, Macmillan Lyimo amepiga kura yake muda mfupi uliopita
    Mgombea urais wa TLP, Macmillan Lyimo amepiga kura yake muda mfupi uliopita, asema hapakuwa na fomu namba 19 lakini kitambulisho alikuwanacho.

  • October 20, 2015

  • WENYE SIMU ZA WHATSAPP, BLOGGERS, VYOMBO VYA HABARI HII INAWAHUSU SIKU YA UCHAGUZI TCRA YATOA ONYO



    WENYE SIMU ZA WHATSAPP, BLOGGERS, VYOMBO VYA HABARI HII INAWAHUSU SIKU YA UCHAGUZI TCRA YATOA ONYO

    Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui na Maadili wa TCRA, Injinia Margaret Munyagi (katikati) akifafanua jambo
    MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevionya vyombo vya habari vitakavyotangaza matokeo ya uchaguzi mkuu kinyume cha sheria na taratibu kwamba haitasita kuviadhibu. Anaandika Charles William … (endelea).
    Mbele ya wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya maudhui ya vyombo vya habari, Injinia Magreth Munyagi ameonya kuwa utangazaji wa matokeo ya uchaguzi kabla ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ambao umekuwa ukizungumzwa na baadhi ya wanasiasa lazima uzingatie taratibu zilizowekwa na tume tofauti na hapo hatua kali zitachukuliwa na TCRA.
    Kumekuwa na mvutano baina ya Tume na vyama vya upinzani hususani vile vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuhusu utangazaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka huu huku Tume ikisisitiza kuwa ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza matokeo na vyama hivyo vikisema hakuna sheria inayovizuia kutangaza matokeo ya vyama vyao.
    Wiki tatu zilizopita, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bara), John Mnyika alisema "hakuna sheria inayotuzuia kutangaza matokeo ya kura zetu na ndio maana tunasisitiza tutayatangaza matokeo yetu wenyewe iwapo tutamaliza kujumlisha kabla ya masaa 72 ambayo NEC inasema itakuwa imemaliza."
    Akijibu swali la MwanaHALISI Online iwapo vyombo vya habari kutangaza matokeo yatakayokuwa yametolewa na chama au vyama vya siasa ni kosa kisheria, Injinia Munyagi amesema "Tumeshaeleza kwamba utangazaji matokeo lazima uzingatie sheria na taratibu za NEC."
    Baadhi ya adhabu zilizotajwa kutumika kwa atakayethibitika amevunja sheria ni kuonywa, kupigwa faini, kufungiwa kwa muda na kunyang'anywa leseni ya utangazaji.
    Pia Mamlaka kupitia kamati hiyo ya maudhui ya vyombo vya habari, imeeleza kuridhishwa kwa 'wastani' na utolewaji wa matangazo ya habari za kampeni.
    "Mpaka sasa tumeridhishwa kwa wastani na kazi iliyofanywa na vyombo vya habari katika kampeni za uchaguzi mkuu, taarifa za uchochezi na kutia hofu zimepungua na waandishi wanajitahidi kutafuta vyanzo sahihi vya habari zao," ameeleza mwenyekiti injinia Munyagi.
    Kamati ya Maudhui huteuliwa kisheria na waziri mwenye dhamana ya masuala ya habari jukumu kubwa la kamati hiyo likiwa ni kufanya tathimini za mara kwa mara kuhusu maudhui ya utangazaji na kupokea maoni au malalamiko juu ya maudhui ya vipindi hivyo.


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.