September 09, 2015

  • WANAOSOMESHWA KWA ADA NAFUU WAMIMINIKA



    WANAOSOMESHWA KWA ADA NAFUU WAMIMINIKA
    Baadhi ya wanachuo wa Mlimani School of Professional Studies cha jijini Dar es Salaam, wakiwa darasani.
    Na Mwandishi Wetu
    Vijana kutoka mikoa mbalimbali wamezidi kumimika kutumia fursa ya kujipatia masomo ya ngazi ya chuo inayotolewa na Chuo cha Mlimani School of Professional Studies cha jijini Dar es Salaam.
    Mkurugenzi wa chuo hicho Hassan Ngoma alisema idadi ya wanaojitokeza kujiunga na mpango huo maalumu wa kuwasaidia maskini kupata elimu bora ni kubwa na kwamba imekuwa ikiongezeka kila siku.
    "Tuliweka kiwango fulani cha kusaidia watu, lakini kutokana na mahitaji ya wanafunzi tumeona tuongeza kidogo, watakaowahi tutaendelea kuwapokea mpaka uwezo wetu utakapokomea.
    "Kama nilivyosema, lengo la chuo chetu ni kuwasaidia vijana wapate elimu siyo kutengeneza faida kubwa. Ndiyo maana tumekuwa tukitoa taaluma mbalimbali pamoja na kuwasaidia wanafunzi wetu kupata ajira," alisema Hassan.
    Aidha, Hassani alizitaja baadhi ya kozi zinazotolewa katika mpango huo wa kusaidia jamii kuwa ni pamoja na Business Administration, Banking and Finance, Accountancy, Human Resource Management.
    Nyingine ni Procurement and Supply, Journalism and Mass Communication na Information Technology.Wanaotaka ufafanuzi wanaweza kupiga simu namba 0715-200900.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.