Akiwa kwenye mkutano wa kampeni Uwanja wa Mkendo, wilayani Musoma, Mkoa wa Mara, amesema yapo mambo mengi hayapendi kwa sababu yanawaumiza wananchi na akichaguliwa kuwa rais atayabadilisha.
Ameutaja mradi wa maji uliopangwa kutekelezwa kupitia ziwa Victoria, aliosema kila siku unatajwa lakini hautekelezwi huku wananchi wa Mkoa wa Mara wakiendelea kupata shida ya maji.
Amesema haina maana kuwa na Waziri wa Maji wakati kunakuwa na mradi usiokwisha, akiwahakikishia wananchi kuwa atakapokuwa Rais, hawezi kushindwa kupata Sh. Bilioni 44 za kutekeleza mradi huo.
Dk. Magufuli ambaye amekuwa waziri katika serikali ya CCM kwa muda mrefu tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza naibu waziri wa ujenzi mwaka 1995.
Kufufua viwanda vilivyo uliwa na watu kwa makusudi ambako kulikuwa na viwanda vingi ambavyo vimekufa mikononi mwa serikali ya CCM
"Naombeni kura zenu wananchi wa Musoma ili tuwatoe watu waovu kwani Serikali haitoki, watatoka watu wabaya ambao nitawatoa haraka sana," amesema.
0 comments:
Post a Comment