September 04, 2015

  • MWANASHERIA WA WIZARA YA MAWASILIANO ASISITIZA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO



    MWANASHERIA WA WIZARA YA MAWASILIANO ASISITIZA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO
    Mwanasheria wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (MCST), Eunice Masigata akitoa ufafanuzi kwenye kikundi juu ya matumizi sahihi ya sheria za mitandao.
    Baadhi ya wananchi na wanahabari wakimsikiliza kwa makini.
    Mafunzo yakiendelea kutolewa juu ya matumizi sahihi ya sheria za mitandao.
    Mmoja wa wanahabari akiuliza swali.
    MWANASHERIA wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Tanzania, Eunice Masigata amewaasa wananchi na wanahabari juu ya matumizi sahihi ya mitandao.
    Akizungumza na wananchi pamoja na wanahabari waliohudhuria kwenye Tamasha la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika Viwanja vya TGNP vilivyoko Mabibo jijini Dar es Salaam, Eunice amewaonya wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao kuhakikisha wanazingatia sheria zilizowekwa.
    Alizitaja baadhi ya sheria hizo kuwa ni pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao, Sheria ya Miamala ya Kielektroniki na Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi inayomwezesha mtu kuficha siri zake.
    Alisema kuwa wataalamu mbalimbali kutoka nje ya nchi na Tanzania mwaka 2013, walikaa pamoja na kuzungumzia masuala ya mitandao juu ya kutumia mitandao kwa matumizi yaliyo bora.
    Aidha, alisema kuanzia Aprili, mwaka huu hadi sasa, wamekuwa wakitoa elimu juu ya matumizi sahihi na namana ya kutekeleza masharti ya ukiukwaji wa sheria hizo.Tamasha hilo lilianza Septemba Mosi, mwaka huu na linatarajiwa kumalizika hapo kesho huku mada kuu ikiwa ni Mageuzi ya Mifumo Kandamizi Hayaepukiki.

    (NA DENIS MTIMA/GPL)


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.