KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis jana alieleza mabadiliko mapya yanayolenga kuwarahisishia Wakatoliki kuvunja ndoa zao na kuoa upya.
Dhamira hiyo ni ishara nyingine ya dhamira ya Papa              huyo kutaka kulifanya Kanisa Katoliki liwe rafiki zaidi na              kuendana matakwa ya walio wengi.
        Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Papa alisema si              haki kwa wenzi kuishi muda mrefu 'wakikandamizwa na wingu la              shaka' kuhusu uhalali wa ndoa zao.
        Ikumbukwe kwamba ni msimamo wa Papa kumkatalia              Mfalme Henry the VIII wa Uingereza kumtaliki mkewe Catherine              wa Aragon katika karne ya 16 uliosababisha England ijitenge              na Rome na kushuhudia kuundwa kwa Kanisa la England huku              mfalme akiwa mlinzi wa Imani wa kanisa hilo.
        Mabadiliko makuu matatu aliyotangaza  Papa jana              ni   kuondoa mchakato wa mapitio ya mara ya pili wa uamuzi              wa kutoa talaka kupitia mahakama ya kanisa kabla ya ndoa              kuvunjwa.
        Mengine ni kuwapatia maaskofu uwezo wa kuharakisha              na kuvunja ndoa   wenzi wanapoamua wenyewe katika mazingira              fulani kama vile ukatili katika ndoa au uasherati na              mchakato huo wa talaka kuwa bure, isipokuwa kwa kulipa ada              ndogo kwa ajili ya gharama za  utawala.
        Kabla ya sheria hiyo, Wakatoliki waliotaka talaka              walihitaji kibali kutoka kwa mahakama mbili za kanisa,              wakati sheria mpya inabakiza moja ingawa rufaa bado              zinaruhusiwa.
        Kabla ya sheria hiyo, wanandoa wa Wakatoliki              wanaotalikiana bila idhini ya kanisa na kuolewa upya              walihesabiwa kama wazinifu na hawakuruhusiwa kupokea              komunio.
        Lakini kwa mujibu wa  utaratibu mpya,              wanaotalikiana wakioa au kuolewa tena watabakia kuwa wafuasi              wa kanisa hilo.
        Mwaka jana Papa aliunda tume ya wanasheria wa              kanisa hilo  kuboresha na kurekebisha taratibu hizo               kurahisisha wanandoa kuachana na kupunguza gharama.
        Mageuzi hayo yalikuja katika mfumo wa nyaraka mbili              zinazoitwa 'motu proprio', neno la kilatini lililobuniwa na              Papa mwenyewe.
        Taratibu hizo zitakuwa rasmi kama sehemu ya sheria              za kanisa (canon law) ifikapo Desemba 8 mwaka huu wakati              Papa atakapoanza kutangaza Mwaka wa Jubilee ambao kwa              kawaida huhusishwa na msamaha.
        
0 comments:
Post a Comment