Watu zaidi ya 54 wameuawa kwenye milipuko mitatu ya            mabomu katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa            Nigeria.
        Msemaji wa jeshi la nchi hiyo amesema kundi la            Kiislamu la Boko Haram, lililoasisiwa Maiduguri, lilihusika.
        Polisi wameambia shirika la habari la Reuters watu 90            walijeruhiwa kwenye mashambulio hayo.
        Mwandishi wa BBC Will Ross anasema sasa ni wazi kwamba            mashambulio hayo ni mojawapo ya mashambulio mabaya zaidi            kutekelezwa miezi ya hivi karibuni.
        Bomu moja lililipuka katika msikiti, na mengine mawili            yakalipuka eneo ambalo watu hukusanyika kutazama mechi za            kandanda, msemaji wa shirika la kutoa huduma za dharura            Muhammad Kanar amesema.
        Milipuko hiyo Maiduguri inaashiria "kiwango cha juu            cha kutamauka" katika Boko Haram, msemaji wa jeshi Sani Usman            alisema kupitia taarifa.
        Kundi hilo limekuwa likitaka kutekeleza uongozi wa            Kiislamu kwa kutumia sharia maeneo ya kaskazini mashariki.
        Watu milioni mbili wamefurushwa makwao tangu            wapiganaji hao waanze harakati zao 2009.
        BBC.
        
0 comments:
Post a Comment