September 10, 2015

  • JAPAN YAKUMBWA NA MAFURIKO MAKUBWA




    JAPAN YAKUMBWA NA MAFURIKO MAKUBWA
    Image copyrightReuters
    Image captionMafuriko nchini Japan
    Mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi nchini Japan vimewalazimisha zaidi ya watu elfu 90 kuzihama nyumba zao.


    Picha zilizochukuliwa kutoka maeneo yaliyoathiriwa kutoka miji ya Joso na Tokyo, zinaonyesha nyumba zilizoharibiwa na mafuriko hayo.
    Wazee walionekana wakipanda kwenye paa za nyumba kabla ya helikopta za kikosi cha uokozi kuwanusuru.
    Nyumba zote na magari vimesombwa na maji ya mto ujulikanao kama Kinugawa baada kingo zake kupasuka kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa siku tatu.
    Takriban watu 12 wamejeruhiwa huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.
    Kumekuwa na hofu kwamba huenda maji ya mafuriko hayo yakasomba sumu za kemikali ndani ya bahari kwenye mtambo wa nishati ya nuklia wa Fukushima.

    Image copyrightAP
    Image captionNyumba zilizofunikwa na maji


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.