September 27, 2015

  • Mgombea Chadema atiwa mbaroni Dodoma Akituhumiwa Kumpiga Chupa Polisi




    Mgombea Chadema atiwa mbaroni Dodoma Akituhumiwa Kumpiga Chupa Polisi

    JESHI la polisi mkoa wa Dodoma linamshikilia Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema, Benson Kigaila pamoja na wenzake kumi ambao ni wafuasi wa chama hicho.
     
    Kauli hiyo ya kukamatwa kwa wafuasi hao pamoja na mgombea ubunge huyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi, David Misime alipokuwa akizungumza waandishi wa habari.

    Misime alisema Kigaila na wenzake kumi wanadaiwa kukamatwa kutokana na kufanya maandamano bila kibali na kuzuia watumiaji wengine wa barabara kushindwa kuendelea na shughuli zao.

    Mbali na kufanya maandamano bila kibali jeshi la polisi linadai kuwa wafuasi wa Chadema walimshambulia askali polisi kwa kutumia chupa ya soda kumpiga nayo kichwani sambamba na kufanya fujo kituoni.

    Misime alisema matukio hayo yalitokea juzi majira ya saa 12:45 kutokea barabara ya Jamatini na kituo cha polisi baada ya mgombea ubunge wa chadema kumaliza mkutano wake wa kampeni katika eneo la stendi kuu ya Dodoma.

    Misime aliwataja waliokamatwa kuwa ni Benson Kigaila mgombea ubunge Chadema, Khadija Maula, Godfrey Manyanya mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Dodoma.

    Wengine ni Stellah Masawe, Hashimu Kilaini, Alex Thomasi, Prisca Mgaza, Luckyson kweka, Aisha Urio, Pompey Remijo na Lawi Tumuza.

    Kamanda alisema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi wanaandaliwa jarada kwa ajili ya kuwapandisha kizimbani  leo.

    Kutokana na hali hiyo kamanda Misime alisema kuwa jeshi litaendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua wanasiasa ambao watafanya kampeni zao ambazo ni za kuvunja amani.

    Hata hivyo Misime hakuweza kumtaja jina askari aliyedaiwa kujeruhiwa na chupa kichwani na wala hakutaka waadishi wakutane na askari huyo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.