Kamati ya Miss Tanzania                inapenda kuwatangazia wadau wote wanaotaka kuandaa                Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016                kutuma maombi yao ya uwakala kuanzia sasa hadi tarehe 30                Novemba 2015 ndio mwisho wa kupokea maombi hayo. 
        Mashindano yatakayo                fanyika ni ya mikoa tu, hakutakuwa na mashindano katika                ngazi ya wilaya wala Kanda. 
         Sifa za kuwa Wakala wa                Miss Tanzania ni pamoja na:
         1) Uwe na Kampuni                iliyosajiliwa na Mamlaka husika ya Serikali. 
        2) Uwe na mtaji wa                kutosha. 
         3) Uwe na uwezo wa                kuandaa shindano katika ufanisi mkubwa. 
         4) Uwe mstari wa mbele                katika kukuza sanaa za utamaduni nchini. 
         Wakala atakaye pitishwa                na Kamati ya Miss Tanzania atapaswa kujisajili Baraza la                Sanaa la Taifa.(BASATA) kabla hajapewa kibali cha kuandaa                shindano. Wilaya za Mkoa wa D'salaam, Ilala, Kinodoni na                Temeke zitapewa hadhi ya Kimkoa, ikiwa ni pamoja na Mkoa                wa Elimu ya Juu. 
         Ada ya Uwakala ni                shilingi milioni moja. 
         Ada ya Uwakala italipwa                kwa Kamati ya Miss Tanzania baada ya maombi kukubaliwa na                kupitishwa. Maombi yatumwe kwa barue pepe                misstanzania2015@yahoo.com 
        
0 comments:
Post a Comment