September 22, 2015

  • DAR YASHIKA NAFASI YA SITA MAAMBUKIZI YA VVU AFRIKA


    DAR YSHIKA NAFASI YA SITA MAAMBUKIZI YA VVU AFRIKA
     



    Takwimu hizo zipo kwenye ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) uliofanywa kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kuangalia namna jamii za watu wa maeneo ya bandari walivyo na uwezekano wa kupata maambukizi mapya ya ugonjwa huo kutokana na mwingiliano wa mataifa mbalimbali.
    Mshauri wa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Ukimwi (UNAIDS), Marie Engel katika uwasilishwaji wa ripoti hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salam alisema ingawa maambukizi yamepungua nchini, bado Dar ni miongoni mwa majiji yaliyoathirika zaidi.
    "Dar es Salaam ni jiji la sita kati ya 10 yaliyoathirika zaidi Afrika ikiwa na asilimia 6.2 za maambukizi mapya kwa mwaka. Maambukizi ya ndani yamepungua kwa kiasi na mpaka mwaka jana yalikuwa asilimia tano maeneo ya mjini na 7.2 vijijini huku wastani kwa nchi nzima ukiwa asilimia tano," alisema Marie.
    Alifafanua kwamba vita dhidi ya ugonjwa huo vinaendelea na kwamba jamii ya kimataifa inaamini mpaka mwaka 2030 utakuwa historia ingawa kuna kazi kubwa inahitaji kufanywa ili kufikia lengo hilo la kuukabili Ukimwi ulianza kuenea miaka ya 1980.

    MWANANCHI.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.