September 11, 2015

  • Mwalimu afa kwa kuchomwa kisu, kisa wivu wa mapenzi




    Mwalimu afa kwa kuchomwa kisu, kisa wivu wa mapenzi
    Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani


    WATU wawili wamekufa katika matukio mawili tofauti mkoani Kilimanjaro, likiwamo la mwalimu wa shule ya sekondari Minja wilayani Mwanga, Tumaini Magila (27) kumuua mumewe Sweetbert Magila (48) kwa kumchoma kisu, kutokana na wivu wa kimapenzi.
    Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema jana kuwa tukio hilo limetokea Septemba 8 majira ya saa 2.20 usiku eneo la Masumeni kata ya Kifula Tarafa ya Ugweno wilayani humo, ambako ni nyumbani kwa wanandoa hao.
    Kamanda alidai kuwa Sweetbert ambaye pia ni mwalimu wa shule hiyo, aliuawa na mkewe baada ya kuwapo kwa ugomvi wa mara kwa mara huku Tumaini akimtuhumu mumewe kujihusisha na mahusiano nje ya ndoa.
    Alisema siku ya tukio, wanandoa hao walitoka kwa pamoja kwenda kupata vinywaji katika baa iliyopo karibu na makazi yao na waliporejea nyumbani, ulizuka ugomvi miongoni mwao na kuanza kupigana, ikiwemo kutumia visu.
    Ngonyani alisema katika ugomvi huo, Tumaini alichukua kisu na kumchoma mumewe katika paja la mguu wa kushoto na kusababisha kutokwa na damu nyingi, hali iliyochangia kifo chake. Mke huyo hakujeruhiwa.


    "Baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitoroka, lakini polisi kwa kushirikiana na wasamaria wema tulifanikiwa kumkamata Septemba 9 eneo la Buju alipokuwa amejificha… mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani," alisema.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.