Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

September 29, 2015

  • JAJI LUBUVA ASEMA MADAI YA MBOWE HAYANA UKWELI


    JAJI LUBUVA ASEMA MADAI YA MBOWE HAYANA UKWELI
    Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekanusha tuhuma kuwa baadhi ya wakurugenzi wa NEC wameachishwa kazi ghafla na kazi zao wamepewa watu ambao watakipendelea Chama cha Mapinduzi.

    Mwenyekiti wa Tume Jaji Lubuva amesema tuhuma zilizoibuliwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe hazina ukweli wowote na zinapotosha Umma.
    Mbowe alisema kuwa maafisa wa Usalama wa Taifa wamepewa nafasi za uongozi ndani ya NEC
    Jaji Lubuva amesema kuwa kuna mabadiliko yalifanyika mwezi uliopita ambapo Rais Kikwete alimteua Julius Malaba kuwa Mkurugenzi mpya wa Uchaguzi kwa lengo la kuimarisha utendaji wa Tume na sio vinginevyo.
    Jaji Lubuva ameomba baadhi ya viongozi wa kisiasa kuacha kuipotosha jamii


  • FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU



    FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU
    NA JAMIIMOJABLOG)
    WATU wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba
    JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI????!!
    ~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na Inje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.

    ~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
    ~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50
    AINA ZA BAWASIRI
    ~Kuna Aina mbili za bawasiri
    (A) BAWASIRI YA NDANI
    ~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
    ~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
    ~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne
    (1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika
    (2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.
    (3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.
    (4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi
    (B)BAWASIRI YA NNJE
    ~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS
    CHANZO CHA TATIZO
    ~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
    👉KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
    👉KUHARISHA KWA MUDA MREFU
    👉TATIZO LA KUTOPATA CHOO
    👉MATATIZO YA UMRI
    👉KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
    👉UZITO KUPITA KIASI
    👉MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU
    DALILI ZA BAWASIRI
    👉Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
    👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
    👉kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
    👉kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
    👉kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
    MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI
    ~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo Hilo
    ~Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia
    👉KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
    👉KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku
    👉EPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU
    MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI
    👉kupata upungufu wa damu (anemia)
    👉Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo
    👉hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
    👉kuathirika kisaikolojia
    👉kukosa moral ya kufanya Kazi kutokana na maumivu makali
    WASILIANA KWA 0717035770 AU 0753692612.


  • September 28, 2015

  • MBINU 5 ZA KUKUPA MAISHA YA MAFANIKIO



    MBINU 5 ZA KUKUPA MAISHA YA MAFANIKIO



    Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa  ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanininyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu Fulani kufanikiwa.



    Kawaida, katika maisha kama ulivyomchezo wa miguu, au michezo mingine mara nyingi huwa zipo mbinu za kufanikisha kile tunachokifanya. Mbinu hizi huweza kutambulika kama sheria, kanuni, au siri lakini zote hulenga kukufanikisha kama unataka mafanikio ya kweli. Mbinu hizi zinapotumiwa kwa bahati mbaya au nzuri huwa hazifanyi ubaguzi zinamwendea yoyote na kuleta matunda unayoyataka. Hata kama ikitokea umezitumia mbinu hizi kwa bahati mbaya bila kujijua ni lazima utafanikiwa katika maisha yako.

    Mbinu hizi ndizo wanazozitumia wengi wenye mafanikio na kuwafanikisha, ingawa huwa sio kwao kuwa rahisi kukwambia mbinu hizo. Haijalishi unaishi kwa sasa maisha gani au upo kwenye matatizo mengi vipi, ukizitumia mbinu hizi, zitakufanikisha na kukupa maisha ya mafanikio unayoyataka. Acha kulalamika tena na kuishi bila amani. Sasa unaweza ukawa na mafanikio makubwa kama hao unaowaona wamefanikiwa, ikiwa utatumia mbinu hizi kukufanikisha. Unajua mbinu hizi ni mbinu zipi?

    Hizo Ndizo Mbinu 5 Za Kukupa Maisha Ya Mafanikio:-

    1. Kuwa na nidhamu binafsi.

    Ili kupata mafanikio makubwa unayoyahitaji sio suala la kufanya kazi kwa bidii tu, zaidi unachohitaji nikuwa na nidhamu binafsi ambayo itakuongoza kwenye malengo yako. Watu wengi hawana nidhamu binafsi kitu ambacho kinapelekea wengi ndoto zao zinaishia kati. Ni muhimu kuelewa kuwa ni lazima kufanya mambo yale yanayoendana na ndoto zako, hata kama kuna wakati unajihisi umechoka unalazimika kujikaza kufanya jambo hata dogo ambalo litakufikisha kwenye malengo yako. Ukishindwa kuwa na nidhamu binasi katk maisha yako elewa kuwa utashindwa kufikia mipango na malengo iliyo jiwekea.


    2. Jifunze kila mara kwa watu waliofanikiwa.

    Hii itakusaidia kujua vitu vingi usivovijua kuliko kukaa na kung'anga'nia mbinu zilezile ambazo hazikusaidii. Yapo mambo mengi sana usiyoyajua ambayo yanakufanya ushindwe kufanikiwa. Ikiwa utakuwa na uwezo wa kujifunza kwa wale waliofnikiwa utakuwa upo kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa na kusonga mbele. Maisha yako yanazidi kuwa magumu siku hadi siku, kutokana na kukosa kujifunza kwa wengine kwa kujua hilo badili mwelekeo wako na kuwa mtu wa kujifinza mwisho wa siku mafanikio yatakuwa makubwa kwako.

    3. Jifunze kutokana na makosa uliyofanya.

    Inawezekana kuna mahali utakuwa umekosea kwa namna moja au nyingine,badala ya kulaumu na kuumia moyo sana jifunze kutokana na hayo makosa liyoafanya ili isije ikawa kwako rahisi kufanya makosa yaleyale kwa mara nyingine. Ikiwa utajifunza kutokana na makosa na kufanyia kazi kile ulichojifunza hapo utakuwa umechukua hatua moja muhimu ya kuweza kukusaidia kusonga mbele kuyafata mafanikio unayoyataka. Unataka mabadiliko makubwa katika maisha jifunze kutokana na makosa yako na acha sana kulaumu.

    4. Jenga tabia ya kujisomea kila siku.

    Hili ni jambo ambalo nimekuwa nikiliongelea sana kuhusu huu umuhimu wa kujisomea. Unapojisomea unapata vitu vingi sana tena ndani ya muda mfupi. Kupitia huko utaweza kujifunza mambo mazuri yatakayoweza kubadili maisha yako kwa sehemu kubwa na kuwa mtu, tofauti kabisa. Acha uvivu jifunze vitu vipya kila siku. Unaweza ukajifunza kupitia vitabu, ama mitandao mizuri inayoelimisha kama huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kupata maarifa bora na sahihi kabisa. Unapojifunza inakusaidia kukabiliana na changamoto nyingi, ambapo kwako ingekuwa ngumu kuzikabili.

    5. Kuwa na mahusiano sahihi na watu waliofanikiwa.

    Katika kutafuta mafanikio ni vizuri ukawa na mahusiano ama mtandao na watu sahihi ambao watakusaidia kukufikisha kwenye lengo ulilojiwekea. Haina haja kuwa na watu ambao hawakusaidii kutimiza malengo yako. Watu hawa watakukwamisha na kukurudisha nyuma katika maisha yako tu siku zote. Jenga tabia ya kuwa na watu sahihi ambao utajifunza kitu kwao, utashirikiana nao na kujifunza mambo mengi huko ya mafanikio na hatimaye utamudu kusonga mbele.

    Unaweza kubadili maisha yako, kama utafanyia kazi mbinu hizi. Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, karibu katika mtandao huu wa DIRA YAMAFANIKIO uendelee kupata maarifa bora yatakayoweza kuboresha yako, kwa pamoja tunaweza.

    DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

    IMANI NGWANGWALU,

    0713 048 035/dirayamafanikio@gmail.com  


  • September 27, 2015

  • STOP PRESS: TANZANIA YAPETA TENA KATIKA MPANGO WA KUPATA MABILIONI YA MCC



    STOP PRESS: TANZANIA YAPETA TENA KATIKA MPANGO WA KUPATA MABILIONI YA MCC
    ·          Tanzania imetimiza masharti yote ya kupatiwa raundi ya pili ya fedha za maendeleo kutoka Shirika la Maendeleo ya Milenia la Millennium Challenge Corporation (MCC) la Marekani na itaanza kupata na kunufaika na mabilioni hayo ya fedha baada ya wajumbe wa Bodi ya MCC kupiga kura ya kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo chini ya Mpango wa MCC-2.
    Habari hizo njema zimetangazwa Jumamosi, Septemba 26, 2015, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, na Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York, na kuhudhuriwa na watumishi waandamizi wa MCC akiwamo Bwana Kamran Khan, Makamu wa Rais wa Operesheni za MCC. Rais Kikwete yuko New York kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
    "Hongera Mheshimiwa Rais kwa sababu nchi yako, Tanzania imetimiza masharti yote ya kupata fedha nyingine chini ya mpango wa MCC - 2, ikiwa ni pamoja na uongozi wa MCC kuridhika kuwa Tanzania inachukua hatua za dhati kupambana na rushwa," Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete na viongozi wengine wa Tanzania akiwamo Waziri wa Nchi za Fedha wa Zanzibar, Mheshimiwa Yusuf Omar Mzee.
    Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete kuwa Bodi ya MCC, katika mkutano wake wa Septemba 17, mwaka huu na chini ya Mwenyekiti wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bwana John Kerry, imeafiki kuhusu kipengele pekee kilichokuwa kimebakia katika masharti ya kupata fedha za MMC kuwa ni kweli Tanzania inakabiliana ipasavyo na rushwa na kuchukua hatua stahiki kukabiliana na janga hilo la rushwa.
    MCC imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa Tanzania imetimiza masharti ya kuiwezesha kufaulu kupata raundi ya pili ya fedha za maendeleo na pia imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa ni kweli Bodi ya MCC imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa kukabiliana na rushwa.
    Tofauti na fedha nyingi zinazotolewa na wafadhili wengi duniani, fedha za MCC hazitakiwi kurudishwa na nchi inayopewa fedha hizo na pia nchi husika hupewa uhuru wa kuchagua aina ya miradi ya maendeleo ambayo inaitaka igharimiwe na fedha hizo.
    Miongoni mwa wajumbe wengine wa Bodi ya MCC ni pamoja na Waziri wa Fedha wa Marekani ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Mwakilishi wa Biashara wa Marekani duniani, Mwendeshaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), nafasi ambayo kwa sasa anaikaimu Bwana Alfonsi Lenhardt, Mtendaji Mkuu wa MCC Bi. Hyde na Rais wa Taasisi ya International Republican Institute (IRI) Balozi Mark Green.
    Mabalozi Lenhardt na Green walikuwa mabalozi wa Marekani katika Tanzania wakati wa majadiliano, upitishaji na utekelezaji wa MCC–1.
    Bi Hyde amesema sasa linalobakia ni kwa wajumbe wa Bodi kupelekewa muhtasari wa kuidhinisha mabilioni hayo kwa Tanzania ambayo chini ya mpango wa uwekezaji wa MCC–2 yatakwenda katika kuboresha huduma za umeme katika Tanzania ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme katika vijiji vingi zaidi nchini. Kiasi cha asilimia 46 ya Watanzania kwa sasa wanapata umeme kutoka asilimia 10 ya mwaka 2005 na sehemu kubwa ya asilimia hiyo imetokana na msaada wa MCC-1.
    Chini ya Mpango huo wa pili wa MCC, Tanzania itapatiwa kiasi cha dola za Marekani milioni 472.8 (sawa na sh. bilioni 992.80). Kwa kutilia maanani kiasi cha dola milioni 698 (sawa na sh. trilioni 1.46) ambazo zilitolewa chini ya MCC-1 basi Tanzania itakuwa imepata jumla ya dola za Marekani trilioni 2.45 za maendeleo kutoka Marekani katika kipindi cha miaka 10 tu iliyopita. Fedha za MCC-2 zitaanza kutolewa mwakani, 2016.
    Kiasi kilichotolewa kwa Tanzania wakati wa MCC-1 ndicho kilikuwa kiasi kikubwa zaidi ambacho kimepata kutolewa na Marekani chini ya Mpango huo wa Millennium Challenge Corporation na kwa kupita MCC-2 Tanzania itakuwa ni nchi ambayo itakuwa imepata kiasi kubwa cha fedha za maendeleo chini ya MCC duniani.
    Fedha zilizotolewa chini ya MCC -1 zilitumika kujenga Barabara za Tunduma-Sumbawanga, Tanga-Horohoro na Namtumbo-Songea-Mbinga.
    Aidha, fedha hizo zilitumika kujenga upya mfumo wa huduma za maji kwa ajili ya miji ya Dar es Salaam na Morogoro na zilitumika kusambaza umeme katika vijiji vya mikoa 10 ya Tanzania Bara.
    Fedha hizo vile vile zilitumika kutandaza njia ya pili ya kusafirisha umeme chini ya Bahari ya Hindi kati ya Bara na Tanzania Visiwani na pia zilitumika kujenga barabara zote kuu za Kisiwa cha Pemba na baadhi ya barabara za Unguja kwa kiwango cha lami.

    Imetolewa na:
    Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
    Ikulu,
    DAR ES SALAAM.
    27 Septemba, 2015




  • Mgombea Chadema atiwa mbaroni Dodoma Akituhumiwa Kumpiga Chupa Polisi




    Mgombea Chadema atiwa mbaroni Dodoma Akituhumiwa Kumpiga Chupa Polisi

    JESHI la polisi mkoa wa Dodoma linamshikilia Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema, Benson Kigaila pamoja na wenzake kumi ambao ni wafuasi wa chama hicho.
     
    Kauli hiyo ya kukamatwa kwa wafuasi hao pamoja na mgombea ubunge huyo ilitolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi, David Misime alipokuwa akizungumza waandishi wa habari.

    Misime alisema Kigaila na wenzake kumi wanadaiwa kukamatwa kutokana na kufanya maandamano bila kibali na kuzuia watumiaji wengine wa barabara kushindwa kuendelea na shughuli zao.

    Mbali na kufanya maandamano bila kibali jeshi la polisi linadai kuwa wafuasi wa Chadema walimshambulia askali polisi kwa kutumia chupa ya soda kumpiga nayo kichwani sambamba na kufanya fujo kituoni.

    Misime alisema matukio hayo yalitokea juzi majira ya saa 12:45 kutokea barabara ya Jamatini na kituo cha polisi baada ya mgombea ubunge wa chadema kumaliza mkutano wake wa kampeni katika eneo la stendi kuu ya Dodoma.

    Misime aliwataja waliokamatwa kuwa ni Benson Kigaila mgombea ubunge Chadema, Khadija Maula, Godfrey Manyanya mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Dodoma.

    Wengine ni Stellah Masawe, Hashimu Kilaini, Alex Thomasi, Prisca Mgaza, Luckyson kweka, Aisha Urio, Pompey Remijo na Lawi Tumuza.

    Kamanda alisema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na polisi wanaandaliwa jarada kwa ajili ya kuwapandisha kizimbani  leo.

    Kutokana na hali hiyo kamanda Misime alisema kuwa jeshi litaendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua wanasiasa ambao watafanya kampeni zao ambazo ni za kuvunja amani.

    Hata hivyo Misime hakuweza kumtaja jina askari aliyedaiwa kujeruhiwa na chupa kichwani na wala hakutaka waadishi wakutane na askari huyo.


  • Wahadhiri UDOM kugoma, wadai mishahara



    Wahadhiri UDOM kugoma, wadai mishahara

    WAHADHIRI takriban 800 waliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wameazimia kutoingia madarasani kufundisha kuanzia Novemba 2 mwaka huu mpaka hapo serikali itakaposhughulikia suala la muundo mpya wa mishahara.

    Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanataaluma wa UDOM (Udomasa), Gerald Shija alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya mkutano mkuu wa wanataaluma hao uliofanyika Septemba 21 mwaka huu.

    Amesema kwa pamoja wameazimia na kutoa msimamo huo mpaka hapo serikali itakapotekeleza.

    Kwa mujibu wa Shija alidai kuwa Rais alitoa taarifa kupitia vyombo vya habari Agosti 22 mwaka 2013 ambao uliagiza muundo huo uanze kutumika Julai Mosi mwaka huu lakini mpaka sasa haujaanza.

    Amesema kumekuwepo na mishahara isiyofanana kwa watu wenye elimu inayofanana na kufanya kazi inayofanana na hivyo kutofautiana na sera ya Serikali inayoelekeza kuwa watu wenye elimu inayofanana kulipwa mishahara inayofanana.

    Shija amesema wanaamini kuwa muundo huo wa utumishi ulioanishwa na wanataaluma ndio muundo bora ukilinganisha na muundo unaotumika sasa hivi.

    Aliiomba serikali kutekeleza muundo huo ili kuondoa kero ambazo zilibainishwa kwa Rais, hali iliyomfanya aagize uanzishwaji na utekelezwaji wa muundo huo.

    Aidha amesema hivi sasa hawana imani na viongozi wa serikali kutokana na kutotekeleza muundo huo katika kutatua kero za muundo uliopo hivi sasa.

    "Ucheweleshwaji wa muundo huu umekuwa ukikwamishwa na Hazina, Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na Utumishi wa umma ambapo wamekuwa wakitupiana mpira," amesema Shija.

    Hata hivyo amesema mnamo Desemba 11, 2014, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilitoa waraka kuagiza Vyuo kupitia Ofisi za rasilimali watu kuzingatia utaratibu ulioanishwa katika muundo na wanataaluma ikiwemo masuala ya vyeo na kuajiri kwakuzingatia vigezo na kuwapanga watumishi wanataaluma.

    Naye Katibu Mkuu wa Umoja huo, Lameck Thomas amesema kuwa muundo huo ulilenga kuweka usawa wa maslahi ya watendaji wa Vyuo vikuu na Vyuo vya Umma na vyuo vikuu vishiriki ili wawe sawa lakini hakuna kilichotekelezwa.

    "Kwa kweli nieleze kwa masikitiko makubwa na tusingependa tufikie hatua hii lakini serikali ndio imetufanya tufikie hapa, tutahakikisha tunapigania muundo huu hadi tupate haki zetu kwani ni nyenzo sahihi lakini tatizo la kulipwa mishahara tofauti kwa wahadhiri lipo katika Chuo Kikuu cha Dodoma tofauti na vyuo vingine," amesema Thomas.

    Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati Utendaji ya Udomasa, Mandela Peter amesema bora muundo huo uje ili kuleta usawa kutokana na kutofautiana kwa kiasi kikubwa mishahara kwa wahadhiri wa UDOM na vyuo vingine kama vile Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

    "Yaani ukiangalia katika vyuo vya UDSM, Sokoine, Mzumbe ukilinganisha na UDOM kuna tofauti kubwa kati ya Sh. 700,000 hadi 1,000,000 kwa mshahara anaopokea mhadhiri msaidizi, sasa hapo utaona kutokana na tofauti hiyo ni bora muundo huu uanze kutekelezwa ili tuwe sawa," amesema Mandela.

    Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) katika chuo hicho, Nashon Maisori aliiomba serikali kutopuuza madai hao kwani wasipoyapatia ufumbuzi watasababisha zaidi ya wanafunzi 18,000 kuathirika kutokana na hali hiyo.


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.