UFARANSA imeanza vizuri kampeni zake za kusaka Kombe la Dunia baada ya kuichapa Honduras bao 3-0 katika mchezo wa kusisimua wa kundi E.
Karim Benzema akaibuka shujaa kwa kuipachikia Ufaransa mabao mawili, moja la mkwaju wa penalti na lingine la shuti kali kutoka 'Impossible angle'.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid alifungua kitabu cha magoli kwa njia ya penalti baada ya Wilson Palacios kumfanyia madhambi Paul Pogba. Penalti hiyo iliambatana na kadi ya pili ya njao kwa Palacios na hivyo kufanya Honduras kucheza pungufu tangu dakika ya 42.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya kombe la dunia, teknolojia ya goli ilianza kutumika katika mchezo huu pale ilipoamua kwa utata kuhusu goli la pili.
Ilikuwa hivi: Karim Benzema alipokea krosi ya Cabaye na kuusukumiza mpira wavuni. Teknolojia ya goli ikasema mpira haukuvuka mstari na hivyo si goli lakini iliporudia mara ya pili ikasema ni goli ila halikufungwa na Benzema bali kipa Noel Valladeres amejifunga!
Uchu wa Benzema haujakomea hapo, alipachika bao la tatu dakika ya 71 kwa shuti kali lililomshinda kipa Noel Valladeres.
Ufaransa walikuwa na hali ngumu kipindi cha kwanza ambapo Honduras walihakikisha wanatibua mipango yao yote lakini mambo yakabadilika ukingoni mwa kipindi hicho cha kwanza hususan baada ya kutolewa Wilson Palacios.
Katika mechi hiyo beki wa zamani wa Arsenal Bacary Sagna aliyejiunga na Manchester City alijukuta akisugua benchi mwanzo mwisho.
0 comments:
Post a Comment