ARGENTINA imepata ushindi wa mbinde dhidi ya Bosnia-Hercegovina katika mchezo mkali wa kundi F ulioisha kwa matokeo ya 2-1.
Kikosi hicho cha Argentina kikahitaji msaada wa bao la kujifunga la Bosnia-Hercegovina kupitia kwa Sead Kolasinac dakika ya tatu ya mchezo na kudumu hadi mapumziko.
Katika kipindi cha kwanza supastaa wa Argentina Lionel Messi hakufurukuta kabisa na hata kiungo wa zamani wa Brazil Juninho akasema: "Katika nusu ya kwanza, Messi amekuwa na kiwango kibovu na anapoteza mipira kirahisi, ana hitaji kubadilika".
Na kweli Messi alibadilika kipindi cha pili, goli lake tamu la juhudi binafsi katika dakika ya 65 likawa ndio bao la ushindi kufuatia Vesad Ibisevic wa Bosnia-Hercegovina kupunguza goli moja zikiwa zimesalia dakika sita kabla mchezo haujamalizika.
Argentina: Romero, Zabaleta, Campagnaro, Federico Fernandez, Garay, Rojo, Maxi Rodriguez, Mascherano, Di Maria, Messi, Aguero.
Bosnia-Herzegovina:
Begovic, Mujdza, Bicakcic, Spahic, Kolasinac, Besic, Hajrovic, Pjanic, Misimovic, Lulic, Dzeko.
0 comments:
Post a Comment