June 23, 2014

  • AINA MPYA YA UHALIFU UNAOKUJA KWA KASI NCHINI TANZANIA



    AINA MPYA YA UHALIFU UNAOKUJA KWA KASI NCHINI TANZANIA
    Na Yusuph Kileo

    Miongoni mwa makosa mtandao kuna lijulikanalo kama "Phishing" ambapo kosa hili limekua likidumu kwa muda sasa katika nchi mbali mbali na kwa upande wa Afrika ilizoeleka kuanzishiwa kutokea Naigeria pamoja na Ghana.

    Nchi mbali mbali zimechukulia uhalifu huu kua ni hatari kwani unaweza kuwa na madhara makubwa kwa mtendewa ikiwa ni pamoja na kupelekea kufilisi mtu, kupata taarifa za watu kinyume na sheria/ makubaliano na hata wakati mwingine kupelekea kuleta madhara mengine kama kutumika kuhatarisha mifumo mbali mbali.


    Kwa kuzingatia hili nchi mbali mbali zimekua na sheria kali dhidi ya uhalifu huu , huku nchi za afrika kupitia umoja wa wataalam wa maswala ya usalama mtandao kuanzisha kamati yenye watu maalaum kuangazia macho uhalifu huu na kutoa taarifa huku hatua zikichukuliwa.

    Makampuni ya Ati-vurus nayo yametoa uzito kwenye hili na kuhakiki wanaunda nyezo madhubuti za utambuzi wa aina hii ya uhalifu na mara kwa mara wakiwasilisha ripoti zao.

    Changamoto bado zipo kutokana na upungufu wa uelewa kwa wananchi mbali mbali juu ya uhalifu huu inayo sababisha  waathirika kueendelea kuwa wengi kila kukicha.



    Uchunguzi umeonyesha mara nyingi panapokua na jambo linalo fatiliwa na wengi ndipo wahalifu wanapenyeza hapo na kuanza kusambaza aina hii ya uhalifu. Nimepata kuliandikia hili kupitia taarifa ya Uhalifu unao ambatana na World cup kama inavyosomeka "HAPA" kwa kirefu.


    Kwa upande wa Tanzania pamekua pakizungumzwa mara zote matumizi mabaya ya mitandao, yanapelekea uhalifu mtandao na hatua kali zitachukuliwa kwa wale wote watakao bainika kujihusisha na uhalifu mtandao.




    Ni vizuri tukakumbushana Tanzania imesha kamilisha rasimu ya sheria za mitandao ambazo zitatoa fursa kwa wahalifu kushughulikiwa ipasavyo na hivi karibuni TCRA nayo ilizungumzia mpango wake wa kushughulikia watumiaji vibaya wa mitandao. Hili likiwa linafuatia kampeni yao ya Futa delete kabisa.


    Wakati hili linajiri pamekua na wimbi la wahalifu wa uhalifu huu wa "Phishing" ambapo wana dukua na kuchukua akauti za mitandao za watu na kuanza kusambaza taarifa zitakazo wawezesha kupata taarifa za  wengine na maranyingine wanatengeneza akaunti feki za mitandao wakitumia majina ya watu maarufu na kuanza kuzitumia vibaya.

    Pamekua pakitumiwa majina ya watu mashuhuri na kutumia watu jumbe wakiwataka wa bonyeze link ili kujiunga na huduma kama Vikoba, Pia wamekua wakituma ujumbe wakiwataka watu wafungue tovuti n.k.

    Katika kulikamilisha hili pamegundulika baadhi ya akaunti za watu tayari wameondolewa umiliki na hatimae wahalifu wanazitumia kusambaza uhalifu huu. Pakumbukwe linapokuja swala la usalama mtandao unapo chukua akaunti ya mtu ni kosa moja na unapo itumia vibaya ni kosa jingine lakini pia unapo tumia watu jumbe kubonyeza tovuti yeyote ni kosa jingine.

    Hadi sasa Baadhi wame toa taarifa kuwa akaunti zao zimechukuliwa, mfano kupitia taarifa inayosomeka "HAPA" na huku baadhi wakitengeneza akaunti feki za majina ya watu na wengine kutuma jumbe za Kiswahili fasaha zinazo onyesha uhitaji wa kuendea tovuti mbali mbali.

    TAHADHARI: Kila mmoja anapaswa kua makini na unapo hisi ya kuwa unaweza ukawa muathirika wa uhalifu huu mtandao basi badilisha neno la siri na siku zote jiepushe kujibu au kufata maelekezo yatakayo kutaka ufanye kitu Fulani. Kutoa taarifa kwenye hili kila linapo jitokeza ni muhimu sana ili hatua stahiki zichukuliwe.

    Ili kujua zaidi uhalifu huu na viambatanishi vingine vya uhali unao fanana na huu unaweza kuusoma "HAPA" na pia nime ainisha namna ya kutambua barua pepe na Tovuti zisizo sahihi katika kiambatanisho hapo chini. Jinsi Ya Kutofautisha Tovuti/Barua pepe sahihi na feki by YUSUPH KILEO


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.