Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

June 30, 2014

  • Membe amuaga rasmi Balozi wa Afrika Kusini nchini



    Membe amuaga rasmi Balozi wa Afrika Kusini nchini
    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimkabidhi aliyekuwa Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Mhe. Thanduyise Henry Chiliza zawadi ya picha ya kuchora ya Mlima Kilimanjaro wakati wa hafla ya kumuaga Balozi huyo ambaye amemaliza muda  wake wa kazi hapa nchini. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) Jijini Dar es  Salaam. (Picha na Reginald Philip)

  • WAZIRI WA NCHI AKIZUNGUMZA NA BALOZI WA UJERUMANI



    WAZIRI WA NCHI AKIZUNGUMZA NA BALOZI WA UJERUMANI
    ???????????????????????????????Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dr. Eng. Binilith Satano Mahenge wa (kwanza kushoto) akizungumza na Balozi wa Ujerumani Mr. Hans Koeppel alipomtembelea ofisini kwakwe mtaa wa luthuli jijini Dar es Salaam, kuhusu mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaotarajia kufanyika julai mwaka huu mjini Berlin Ujerumani.???????????????????????????????Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Mazingira Dr. Eng. Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Julius Ningu (wa kwanza kulia) wakiwa pamoja na Balozi wa Ujerumani Mr.  Hans Koeppel kwa ajili ya Mazungumzo jijini Dar es Salaam.


  • MUIGIZAJI WA FILAMU YA TITANIC YUPO BRAZILI NA MELI YA KIFAHARI



    MUIGIZAJI WA FILAMU YA TITANIC YUPO BRAZILI NA MELI YA KIFAHARI
    Dunia yote imeangazia mashindano ya fainali za kombe la dunia na kila mwenye muda na uwezo amefika Brazil kuhakikisha anaangalia kwa moja kwa moja mashindano hayo.
    Mastaa kibao wametua Brazil kwa mitindo tofauti lakini muigizaji wa Titanic Leoonardo DiCaprio ametia fora baada ya kuingia nchini humo akiwa na meli kubwa ya kifahari aliyokodi kwa safari hiyo, meli hiyo inamilikiwa na mmiliki wa Manchester City, Mansour bin Zayed Al Nahyan.
    Meli hiyo imetajwa kuwa na Swimming pool, chumba kikubwa cha mazoezi, jumba la sinema na ukumbi mkubwa wa mikutano ukiacha mbali vyumba vya kulalala na sehemu nyingine.
    Muigizaji huyo amewachukua marafiki zake 21 na wanakula nao maisha katika safari hiyo huku wakishuhudia mechi kadhaa.


  • WATANZANIA WAENDELEA KUMIMINIKA KATIKA BANDA LA PPF SABASABA KUJIPATIA HUDUMA MBALIMBALI



    WATANZANIA WAENDELEA KUMIMINIKA KATIKA BANDA LA PPF SABASABA KUJIPATIA HUDUMA MBALIMBALI
     Afisa Michango kutoka PPF Makao Makuu, Bi Glory Maboya (kulia) akimpatia maelezo ya Huduma mbalimbali mmoja wa wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipotembelea Banda la PPF katika Viwanja vya Mwl Nyerere maarufu kama Sabasaba.
     Mkazi wa Jiji la Dar Es Salaam akipatiwa maelezo juu ya huduma ya Fao la Kujitoa kutoka kwa afisa uendeshaji wa Mfuko wa PPF kanda ya Ziwa, Bi Grace Balele wakati mteja huyo alipotembelea banda la Mfuko wa Pensheni wa PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba.
    Mchambuzi wa Mfumo wa Teknolojia (System Analysist) kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Makao Makuu, Bi Irene Togolai akimpatia fomu ya Kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF mmoja wa Wakazi wa Jiji la Dar aliyetembelea Banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Kibiashara ya Kimataifa yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba
    Mchambuzi wa Mfumo wa Teknolojia (System Analysist) kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF Makao Makuu, Bi Irene Togolai akijibu maswali ya wateja wa PPF waliofika katika banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara za Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl Nyerere Barabara ya Kilwa, Jijini Dar Es Salaam.
     Happiness Mmbando , Afisa Rasilimali watu Utawala na Ushauri kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF akiwasikiliza kwa makini baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar waliotembelea Banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara za Kimataifa.
    Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam wakiuliza maswali kuhusiana na mfuko wa Pensheni wa PPF wakati walipotembelea katika banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar Es Salaam, Kulia ni Afisa Huduma kwa Wateja Kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF kanda ya Temeke, Bi Jacquline Jackson


  • PICHA WANAFUNZI WA UDOM WALIPOKUWA WANAGOMBANIA USAFIRI


    PICHA WANAFUNZI WA UDOM WALIPOKUWA WANAGOMBANIA USAFIRI

     Askari polisi anayelinda usalama wa abiria na mali zao katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani akijalibu kutoa maelekezo kwa wanafunzi wa UDOM waliofika kutafuta usafiri kituoni hapo na kukuta hali ya usafiri hailidhishi kutokana na uchache wa Mabasi.
     Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakigombania kulipa nauli kwa ajenti wa Basi la Urafika linalofanya safari zake kuelekea Iringa  baada ya baadhi ya Vyuo kufungwa kwa pamoja na hivyo kufanya idadi ya abiria wa mikoani kuwa wengi kuliko mabasi yaliyopo.
    Baadhi ya Abiria wakitafakari na mabegi yao baada ya kufika kituo cha mabasi ya kwenda mikoani na kujikuta wakikosa usafiri kutokana na uchache wa mabasi ulisababishwa na vyuo vilivyopo mkoani Dodoma kufungwa kwa wakati mmoja.



    Na John Banda, Dodoma

    DODOMA imekumbwa na uhaba wa usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani kutokana na vyuo vikuu na vile vya kawada kufungwa katika kipindi kimoja hali iliyowasababishia  abiria usumbufu mkubwa ikiwa ni pamoja

    na nauri kupanda kinyemela. Wanafunzi hao hasa wa Vyuo vikuu vya Dodoma (UDOM),  Mtakatifu Yohana, Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) na kile cha Biashara (CBE) ambavyo vina wanafunzi wengi vimefungwa kwa likizo ya miezi mitatu.

    Wakiongea na mwandishi wa habari hizi walipokutwa wamezagaa katika kituo cha mabasi ya kwenda mikoani walisema leo ni siku ya tatu tangu kuusotea usafiri huo bila mafanikio. Neema Binamu alisema kutokana na wanafunzi wa vyuo vyote kukutana kwa pamoja kusaka usafiri imekuwa shida kutokana na Idadi ndogo ya mabasi.
    Hali iliyosababisha wenye magari wasiyowaaminifu kupandisha bei kinyemela mpaka kufikia 30,000 badala ya 17000 na wanapolipa kiasi hicho huandikiwa nauri ya kawaida tofauti na hapo hakuna anaesikilizwa.

    ''Kikubwa ni kwa vyombo vinavyohusika na usafirishaji vinatakiwa kujipanga mapema hasa wakati wa misimu kama hii ambayo vyuo vinafungwa ili kutuepushia usumbufu ambao hata hatujui kama tutondoka au la'',
    alisema
    Kwa upande wao baadhi ya maajenti ambao hawakutaka kuandikwa majina yao walisema vipindi kama hivi ni vya neema kwao kutokana na siku za kawaida kura dagaa na sasa watakura kuku takribani wiki nzima. Nae Mmoja wa askari wa usalama barabarani aliyekuwepo kituoni hapo alisema yeye si msemaji lakini swala Nauri ya mabasi imegwanyika katika Madaraja matatu ambapo ni 23,000 lile la kwanza na 17,000 la
    tatu. Na kuhusu upandishwaji nauri kiholela alisema hilo wanalo na wanawapitia abiria wanaosubili usafiri na kuwapa elimu ili wasilipe zaidi ya nauri iliyowekwa halali. 


  • ROBBEN AKUBALI ALIJIANGUSHA, MASHABIKI MEXICO WACHARUKA




    ROBBEN AKUBALI ALIJIANGUSHA, MASHABIKI MEXICO WACHARUKA
    Kauli ya mshambuliaji wa Uholanzi, Arjen Robben kwamba kweli alijirusha kwenye mechi dhidi ya Mexico imewakera mashabiki wa timu hiyo.
    Robben amesema alijirusha mara kadhaa lakini akakataa kwamba alijiangusha katika dakika ya tatu ya nyongeza iliyozaa penalti.
    Alisema mara zote alizojiangusha hakufanikiwa kumshawishi mwamuzi, lakini mwisho akaangushwa na Klaas Jan Huntelaar akapiga mkwaju wa penalti na kufunga.
    Mashabiki wa Mexico walizichana picha za Robben na kumuita mwizi wengine wakamuita muongo.


  • Umbea wa Nathan Mpangala



    umbea wa nathan mpangala



  • RAIS KIKWETE KUFUNGUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII



    RAIS KIKWETE KUFUNGUA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII
    indexSwahili Tourism Expol kufanyika Dar es Salaam
     
    Na Mwandishi Wetu
     
    RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya kimataifa ya utalii yanayojulikana kama Swahili Tuorism Expo yanayotarajiwa kufanyika Dar es Salaam Oktoba mwaka huu.
     
    Waziri wa Maliasili na Utalii Razaro Nyalandu aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Dar es Salaam alipozindua rasmi tovuti ya taarifa za maonyesho hayo inayojulikana kama Swahili Tourism Expo (S!TE).
     
    Maonyesho hayo yatakayohusisha kampuni binafsi, taasisi za kiserikali kama Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na washirika wengine katika sekta hiyo yanatarajiwa kufanyika tarehe 1 mpaka 4 Oktoba, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. 
    Waziri Nyalandu alisema maonyesho hayo ni fursa ya kipekee kwa Tanzania kupanua wigo wa sekta ya utalii ambapo nchi zote za ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na Sudan zinatarajiwa kushiriki lakini pia mataifa mbalimbali yataalikwa.
     
    Alisema tayari 50% ya nafasi za maonyesho zimeshachukuliwa na kwamba mialiko kwa mataifa mbalimbali imeshatumwa ambapo ofisi yake itafuatilia kwa karibu mialiko hiyo na kuhakikisha nchi nyingi kwa kadri inavyowezekana zinashiriki.
     
    "Kutokana na ukubwa wa tukio hili Rais Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi lakini pamoja na TTB kupewa jukumu la kuratibu pia ofisi yangu itachukua jukumu la kipekee  kufuatilia mialiko iliyotumwa nchi mbalimbali kuhakikisha zinashiriki," alisema Waziri.
     
    Aliongeza kuwa maonyesho hayo yanatarajiwa kuongeza biashara ya kitalii nchini ambapo baada ya hapo Tanzania inatarajiwa kupokea watalii zaidi ya milioni 2 kwani maonyesho hayo yataitangaza nchi husika kwa kiasi kikubwa.
     
    Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB, Balozi Charles Sanga alisema maonyesho hayo yatakuwa chachu ya kukuza utalii wa ndani na kuwajengea tabia watanzania kutembelea vivutio tulivyonavyo.
     
    Alisema tumekuwa tukipokea watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja kujionea utajiri wa maliasili tulizonazo lakini idadi ya watalii wazalendo imekuwa ndogo sana ambapo pamoja na mambo mengine muamko na taarifa za vivutio hivi zimekuwa haziwafikii na hivyo maonesho hayo yatakuwa chachu ya kuongeza idadi ya watalii wa ndani.
     
    "Maonyesho kama haya ni maarufu katika nchi za wenzetu na yamekuwa yanawasaidia sana katika kukuza sekta zao za utalii hivyo nasi tunaanza na litakuwa linafanyika kila mwaka,"
     
    "Kupitia maonyesho haya sekta na biashara nyingi za kitalii zitapanuka lakini kubwa zaidi tunaamini baada ya hapo watanzania wengi watakuwa na taarifa za kutosha kuhusu maliasili tulizonazo na watahamasika na hatimaye kuongeza idadi ya watalii wa ndani ya nchi," alisema Balozi Sanga.
     
    Wizara ya Maliasili kupitia TTB imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa na mchango wa kipekee katika pato la taifa ambapo pamoja na maonyesho hayo pia ina mikataba mbalimbali ya matangazo na nchi mbalimbali duniani katika kuhakikisha taarifa za vivutio vyetu zinawafikia watu wengi zaidi.


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.