Gari la Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, yenye namba T 862 BBC aina ya JEEP, imepata ajali mchana huu katika maeneo ya Nyasubi Kahama, kwenye barabara kuu iendayo nchi jirani za Rwanda na Burundi.
|
Mwenywkiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja |
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, mara baada ya ajali hiyo dereva wa gari hilo ambaye hajafahamika mara moja alikimbia, huku ikiarifiwa kuwa alipata majeraha kidogo kwani gari liliangukia upande wake.
Mtu mwingine ambaye alikuwepo katika ajali hiyo hakupata majeraha yoyote, na kwamba Gari hiyo imeinuliwa na kuondolewa eneo la tukio.
|
Gari hiyo muda mfupi baada ya kuinuliwa kutoka mtaroni |
0 comments:
Post a Comment