Mamlaka ya Chakula na Dawa kanda ya kaskazini imekamata na kuteketeza shehena ya vyakula madawa na vinywaji vyenye madhara kwa wananchi vilivyokuwa vinaendelea kutumika katika maeneo mbalimbali ya kanda hiyo na imewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kukabiliana na tatizo hilo.
Mkurugenzi wa TFDA kanda ya kaskazini Bw,Damasi Matiko amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na mamlaka hiyo tatizo bado ni kubwa na ushirikiano wa wananchi unahitajika ukiwemo wa kuwa makini katika matumizi ya bidhaa zote na kutoa taarifa pindi wanapobaini mapungufu.
Afisa afya wa manispaa ya jiji la Arusha Bw Leny Sumari amesema madhara ya matumizi ya bidhaa bandia ama zilizopita muda wake ni makubwa zaidi kwa watoto na ameikata jamii kuwa makini kwa kuchunguza zaidi bidhaaa zinauzwa kwa bei rahisi.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi akiwemo Bw, Julius Moses ,Peter Ngusa , na Simion Mollel pamoja na kuipongeza TFDA kwa jitihada wanazofanya wamesema bado ziko taasisi nyingine za serikali ambazo hazijatimiza wajibu wake ipasavyo.
chanzo ITV.
0 comments:
Post a Comment