June 23, 2014

  • TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOMBERO , JUNI 2014


    TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOMBERO , JUNI 2014
    Chanzo : Gazeti la  Mwananchi of 23rd June
    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero anawataiqazta wananchi wote wenye sifa, nafasi wazi 9 za kazi. Nafasi hizo nl;-

    Dereva Daraja II - Nafasi 1 - Mshahara TGOS A 
    Sifa:
    • Pwve na leseni daraja la C ya uendeshaji
    • Awe na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali
    • Awe na cheti cha majaribio ya ufundi daraja II.

    Majukumu ya kazi:
    • Ataendesha magari ya abiria (watumishi) au malori
    • Atahakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote na -kufanya uchunguzi kabla na baada ya safari iii kugundua ubovu unaohitaji matengenezo
    • Atafanya matengenezo madogo madogo katika gari na
    • Atatunza na kuandika daftari la safari "log-book" kwa safari zote.

    Msaidizi Wa Kumbukumbu Daraja II - Nafasi 3 - Mshahara TGS B
     Sifa:
    • Awe na cheti cha Utunzaji Kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi
    Majukumu ya kazi:
    • Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji
    • Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka
    • Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki
    • Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka nk) katika mafaili/majalada
    • Kazi nyingine atakazopangiwa.

    2. KATIBU MUHTASI DARAJA III - Nafasi 2 - Mshahara
     Sifa:
    • Awe amehudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu
    • Awe amefaulu soma la hatimkato ya Kiswahili na kiingereza maneno 80 kwa dakika moja
    • Awe amepata mafunzo ya kompyuta kutoka chua cho:hote kinachotambulika na Serikali na kupata cheti katika proqrarn za Windows, Microsoft Office, Internet, E-Mail na Publisher.

    Majukumu ya kazi:
    • Atachapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida
    • Atapokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
    • Atasaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini
    • Atafikisha maelekezo ya mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao

    Fundi Sanifu Msaidizi - Nafasi 1 -Mshahara TGS A
     Sifa:
    • Waliomaliza kidato cha Nne katika masomo ya Sayansi na kufuzu
    mafunzo ya mwaka mmoja katika moja ya fani za Ufundl kutoka Chuo
    kinachotambuliwa na Serikali
    • Waliomaliza Kidato cha Nne wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Hatua ya II kutoka Chuo cha Ufundi katika mojawapo ya fani za ufundi
    Majukumu ya kazi:
    • Kufanya matengenezo ya kawaida (Service) kwa magari na mitambo ya Halmashauri
    • Kuhakikisha kuwa magari na mitambo ya Halmashauri iko kwenye hali nzuri
    • Kukagua magonjwa ya magari na kutoa ushauri kwa fundi mkuu wa magari kuhusiana na ubovu wa magari hayo.

    Mtendaji Wa Kijiji Daraja III - Nafasi 1- Mshahara TGS B 
    Sifa:
    • Awe mwenye elirnu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chua cha Serikali za Mitaa Hombolo, Do:loma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
    Majukumu ya kazi:
    • Afisa Masuull na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijlji
    • Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika kiJiji
    • Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya
    Maendeleo ya Kijiji
    • Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
    • Kutasfiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu
    • Kuandaa taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa,
    umaskini na kuongeza uzalishaji mali
    • Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya kitaalam katika kijiji
    • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za
    kijiji
    • Mwenyekiti wa kikao cha wataalamu waliopo katika kijiji
    • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi
    • Kusimamia utungaji wa Sheria Ndogo za kijiji; na
    • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

    5. MLINZI - Nafasi 1 - Mshahara TGOS A 
    Sifa:
    • Awe amefuzu mafunzo ya Mgambo.Polisi/JKT
    • Awe amemaliza kidato cha nne
    Majukumu ya kazi:
    • Atahakikisha mali vote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati
    ya idhini. Hii ni pamoja na mali Illayoingia.
    • Atalinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku
    • Atahakikisha milango na madirisha ya ofisi yanafungwa mwisho wa saa za kazi
    • Atapambana na majanga yoyote yatakayotokea sehemu ya kazi
    • Pamoja na kazi nyingine za ulinzi atakazopangiwa

    APPLICATION INSTRUCTIONS:

    SIFA ZA JUMLA:
    l. Waombaji wote wawe na umri kati ya miaka 15 - 40
    Wawe wamemaliza Kidato cha Nne au Sita
    Wawe raia wa Tanzania.
    Mwombaji anatakiwa kuwasilisha maombi yake kwa:-

    Mkurugenzi Mtendaji Wilaya,
    S.L.P.263,
    IFAKARA/ KILOMBERO.
    maombi yaambatane na nakala ya vyeti vya shule na vyuo parnoja na picha 2 (passport size)
    Maombl yatumwe kuanzia tarehe 23/06/2014 na mwisho wa kupokea maombi rn tarehe 11/07/2014 saa 9.30 alasiri.
    Azimina Mbilinyi
    Mkurugenzi Mtendaji wilaya
    KILOMBERO.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.