Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Covenant Bi.Sabetha Mwambenja akitoa mfano wa beiskali wakati alipokuwa akiongea na kikundi cha wafugaji Ng'ombe wa kisasa cha Kata ya Somangila Kigamboni jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mradi huo.Benki hiyo inategemea kutoa mkopo kwa kikundi hicho ili waweze kuendeleza ufugaji huo. Kulia ni Mratibu wa Wafugaji wa Ng'ombe wa Kata ya hiyo Getruda Mpelembe na katikati ni mtunza Hazina wa Kikundi hicho Jumanne Hussen na Kushoto ni Mwenyekiti Taifa Wajasiriamali Dk.Dauda Salmin.
Mratibu wa kikundi cha wafugaji wa Ng'ombe wa kisasa Kata ya Somangila Kigamboni jijini Dar es Salaam, Getruda Mpelembe (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Covenant Bi,Sabetha Mwambenja,Baada ya kuongea na kikundi hicho kuhusiana na maswala ya mradi wa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa wa kisasa ambapo kikundi hicho kitanufaika na mkopo kutoka benki ya Covenant kwa ajili ya kuendeleza mradi huo wa ufugaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya wanawake ya Covenant Bi,Sabetha Mwambenja akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiongea na kikundi cha wafugaji wa Ng'ombe wa kisasa cha Kata ya Somangila kiilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mradi wa ufugaji wa kisasa wa ng'ombe wa maziwa unaovihusisha vikundi vitatu vya kata hiyo ambapo wafugaji hao watapata mkopo wa kuendeleza mradi huo kutoka Covenant benki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya wanawake ya Covenant Bi. Sabetha Mwambenja akitoa mfano wa spoko za beiskali kwa kikundi cha wafugaji zaidi ya 45( hawapo pichani)wa Kata ya Somangila kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mradi wa ufugaji wa Ng'ombe wa kisasa wa Maziwa.Benki hiyo inategemea kutoa mkopo kwa kikundi hicho ili kiweze kuendeleza ufugaji huo. Kulia ni mtunza Hazina wa Kikundi hicho Jumanne Hussen.
0 comments:
Post a Comment