June 16, 2014

  • Kanda ya Ilala yapata mabingwa wa Castle Lager Perfect Six




    Kanda ya Ilala yapata mabingwa wa Castle Lager Perfect Six
    Na Mwandishi wetu.

    Kanda ya Ilala imepata wawakilishi kwenye fainali za mashindano mapya ya soka ya Castle Lager Perfect Six baada ya timu ya Barafu FC ya kutwaa ubingwa wa kanda hiyo katika fainali za kanda hiyo zilizopigwa kwenye uwanja wa Nyantale huko Tabata wikendi hii.

    Ubingwa huo kwa timu ya Barafu FC unatoa nafasi ya kuwa mwakilishi kutoka kanda ya Ilala kugombea nafasi ya kwenda nchini Hispania kutembelea uwanja wa Camp Nou na kushuhudia michezo ya klabu ya Barcelona katika La Liga endapo itashika nafasi ya kwanza katika michezo ya fainali ya ngazi ya taifa ya mashindano hayo yatayofanyika jijini Dar es Salaam siku za baadaye baada ya kupata mabingwa kutoka kanda saba.

    Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili baada ya mchezo huo, Meneja wa Bia ya Castle, Kabula Nshimo alisema kuwa katika michezo ya ligi ndogo ya kanda ya Ilala ilikuwa na ushindani mkali kutokana na kila timu kujiandaa kushinda na kuibuka mabingwa katika kanda hiyo ambapo Barafu FC ndiyo mabingwa wa kihistoria katika kanda ya Ilala.

    Nshimo alisema kuwa mechi zilizochezwa wikendi hii zimeonyesha jinsi gani Watanzania wana mwamko na shauku kubwa ya kushiriki mashindano kutokana na watu kujitokeza kwa wingi maeneo mbalimbali ambapo yalifanyika mashindano hayo.

    Nshimo alisema mashindano ya Castle Lager Perfect Six yamelenga kuzungumza na wanywaji wa Castle Lager ambao wana shauku ya kucheza mpira wa miguu, kuleta pamoja wanywaji wa Castle Lager kutoka sehemu mbalimbali nchini ili wafurahie pamoja na kuwapa zawadi wateja hao wa bia hiyo.

    Vilevile wikendi hii yalifanyika mashindano hayo kwenye mkoa wa Mbeya na Kilimanjaro katika hatua za awali kupata wawakilishi watakaocheza fainali za Kanda husika na pia zilifanyika fainali Kanda ya Ziwa ambapo hadi tunaenda mitamboni mashindano yalikuwa bado yanaendelea katika hatua za kupata wawakilishi wa Kanda kwenye fainali za taifa. Mashindano ngazi ya fainali za Kanda yataendelea wikendi ijayo kwenye mikoa ya Kinondoni, Mbeya (Kanda ya Kusini) na Arusha (Kanda ya Kaskazini Mashariki).
    Wachezaji na Mashabiki wa Timu ya Barafu Kona, wakishangili baad ya timu hiyo kuibuka mabingwa dhidi ya Mburahati wakati wa Fainali za Castle Lager Perfect Six kanda ya Ilala zilizofanyika katika Uwanja wa Nyantale Tabata Dar es Salaam leo.
    Wachezaji wa Timu ya Barafu Kona, wakishangilia na kombe lao walolipata baada ya timu hiyo kuifunga timu ya Mburahati magoli 10-2 na kuibuka mabingwa wa Castle Lager Perfect Six kanda ya Ilala katika mchezo mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Nyantale Dar es Salaam.
    Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo wa pili (kushoto) akimkabidhi Kapteni wa timu ya Barafu FC, Moris Kamongo (kushoto), kombe baada ya kutawazwa mabingwa wa Bonanza la Castle Lager Perfect Six katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Nyantale Dar es Salaam jana. Mabingwa hao wataiwakilisha Ilala kwenye fainali za taifa.
    Mchezaji wa Timu ya Mburahati, Fred Denis (kushoto) akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Barafu Kona, Ally Tigana, wakati wa Fainali za Castle Lager Perfect Six kanda ya Ilala zilizofanyika katika Uwanja wa Nyantale Tabata Dar es Salaam jana. Timu ya Barafu ilishinda kwa Magoli 10 -2.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.