August 14, 2014

  • Kesi ya bosi wa bandari na msaidizi wake: upelelezi wakamilika, maelezo ya awali kusikilizwa septemba 11, 2014



    kesi ya bosi wa bandari na msaidizi wake: upelelezi wakamilika, maelezo ya awali kusikilizwa septemba 11, 2014

    Na Sultani Kipingo, Mahakamani
    UPANDE wa Jamhuri katika kesi inayomkabili aliyekuwa  Mkurugenzi wa Mlamkala ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Ephraimu Mgawe na msaidizi wake, umedai kwamba upelelezi umekamilika dhidi ya tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka kwa kusaini mkataba wa kuipa kazi Kampuni ya Ujenzi ya China Communications Ltd bila kutangaza zabuni.
    Madai hayo yalitolewa leo na upande wa Jamhuri katika kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawidhi, Isaya Arufani kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
    Mbali na Mgawe mshtakiwa mwingine ni, Naibu Mkurugenzi Mkuu PTA, Hamadi Koshuma.
    Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Osward Tibabyekomya  akisaidiana na Mwendesha  Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ben Linkolin.
    "Mheshimiwa hakimu upelelezi wa kesi hii umekamilika upande wa Jamhuri tunaomba tarehe ya kusikiliza maelezo ya awali…" alidia mheshimiwa Linkolin.
    Hakimu Arufani alisema mahakama hiyo itasikiliza maelezo ya awali Septemba 11, mwaka huu na dhamana ya washtakiwa inaendelea.
    Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuwa Desemba 5, mwaka 2011 huko TPA, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa mamlaka hiyo kwa nyadhifa hizo, walitumia vibaya madaraka yao.
    Ilidaiwa kuwa washtakiwa walitumia vibaya madaraka yao baada ya kusaini mkataba kati ya TPA na Kampuni ya China Communications na kuipa kazi ya ujenzi wa geti namba 13 na 14 la mamlaka hyo, bila kutangaza zabuni  kinyume cha kifungu cha 31 cha sheria ya manunuzi namba 21 ya mwaka 2004. 
    Washtakiwa walikana mashitaka yao kwa nyakati tofauti.
    Mapema Agosti 23, mwaka 2012 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe, alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu, Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
    Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.