Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Oilcom imezindua promosheni ya jishindie mtungi wa gesi, ambapo wateja wa Vodacom watakaojaza mafuta kwa huduma ya M-pesa kwenye vituo vya kampuni ya mafuta ya Oil Com watajishindia mtungi wa gesi.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hii leo katika kituo cha Oilcom cha mtaa wa Libya jijini Dar es Salaam ,Meneja Uhusiano wa Masuala ya Nje wa Vodacom Salum Mwalim,alisema kuwa promosheni hii imewalenga watumiaji wa mafuta ya magari watakaojaza mafuta kwenye magari yao kwa kutumia huduma ya M-pesa.
"OilCom ni moja ya makampuni ambayo yalijiunga katika mtandao wa M-pesa siku chache zilizopita na tunashirikiana nao katika promosheni hii ambapo wateja watakaojaza mafuta katika vituo vya mafuta vya Oilcom vilivyopo mtaa wa Libya,Kipawa na TMJ wataingia kwenye promosheni hii ambapo droo itakuwa ikifanyika mara moja kwa wiki na mshindi atakayekuwa ameweka mafuta mengi kwenye gari kwa kutumia huduma ya M-Pesa atajishindia mtungi wa gesi wa O-Gesi wenye thamani ya shilingi 52,500"Alisema Mwalim.
Mwalim alisema kwamba promosheni hii itadumu kwa kipindi cha miezi mitatu kwa kuanzia itafanyika katika kituo cha mafuta cha Oilcom cha mtaa wa Libya na mwezi utakaofuata itafanyika katika kituo cha Oilcom cha Kipawa na itamalizikia katika kituo cha mafuta cha Oilcom TMJ.
Kwa upande wake Meneja wa maswala ya kompyuta wa kampuni ya OilCom Abubakar Mwita,ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa kubuni promosheni hii ambayo inahamasisha wateja wa mafuta kutumia huduma ya M-pesa na kuwapunguzia usumbufu wa kutembea na hela mfukoni wanapohitaji kujaza mafuta kwenye magari yao.
Alisema tangu OilCom izindue huduma ya wateja wao kulipia mafuta kwa njia ya M-pesa watumiaji wa huduma hii wamekuwa wakiongezaka siku hadi siku na kuifurahia kwa kuwa inawarahisishia maisha na kuwaondolea usumbufu "Tuko mbioni kuhakikisha vituo vyetu vyote vya mafuta viwe na huduma ya kulipia kwa M-Pesa".Alisema Mwita.
Hivi karibuni kampuni ya Vodacom Tanzania na Oilcom ziliingia ubia ambapo wateja wa pande zote mbili wamewezeshwa kulipia mafuta kwa kupitia huduma ya M-Pesa popote kwenye vituo vya kampuni hiyo ya mafuta. Mpaka sasa huduma hii iko katika vituo vya mafuta vya TMJ Msasani,Kipawa na Oilcom kilichopo mtaa wa Libya na upo mkakati unaoendelea kuhakikisha vituo vyote vya Oilcom nchi nzima vinakuwa na huduma ya kulipia kwa M-Pesa.
Meneja Uhusiano wa Masuala ya Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu promosheni mpya ya jishindie mtungi wa gesi kwa kujaza mafuta kwa Mpesa inayoendeshwa na Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya mafuta ya Oil Com,kulia ni Menaja Msaidizi wa kituo cha Oilcom mtaa wa Libya jijini Dar es Salaam Abubakar Kaburu ,Katikati ni Meneja wa masuala ya kompyuta na ufundi wa Oil com,Abubakar Mwita.
Meneja Msaidizi wa kituo cha Oilcom mtaa wa Libya jijini Dar es Salaam Hussein Kaburu kulia pamoja na Meneja Uhusiano wa Masuala ya Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalim wakionesha moja ya mtungi wa O-Gas utakaoshindaniwa katika promosheni mpya ya jishindie mtungi wa gesi kwa kujaza mafuta kwa M-pesa inayoendeshwa na Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya mafuta ya Oil Com,kushoto ni Meneja wa masuala ya kompyuta na ufundi wa Oil com,Abubakar Mwita(kushoto)
Meneja Uhusiano wa Masuala ya Nje wa Vodacom Tanzania,Salum Mwalimo(kushoto) pamoja na Meneja wa masuala ya kompyuta na ufundi wa Oil com,Abubakar Mwita. Wakionesha waandishi wa habari hawapo pichani moja ya mtungi ambayo itakuwa inatolewa kwa washindi wa promosheni mpya ya jishindie mtungi wa gesi kwa kujaza mafuta kwa M-pesa inayoendeshwa na Vodacom kwa kushirikiana na kampuni ya mafuta ya Oil Com.
0 comments:
Post a Comment