August 30, 2014

  • AFRIKA INACHANGIA ASILIMIA 3 TU YA HEWA CHAFU DUNIANI - WAZIRI MKUU


    AFRIKA INACHANGIA ASILIMIA 3 TU YA HEWA CHAFU DUNIANI - WAZIRI MKUU
    WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema tatizo la mabadilko ya tabianchi ni kubwa sana na kama hazitachukuliwa hatua stahiki Dunia itaisha.

    Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Agosti 29, 2014) wakati akifungua mkutano wa pamoja wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Mazingira ambao ni wajumbe wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Barani AfrikainayosimamiaMabadiliko ya Tabianchi (Committee of African Heads of States and Governments on Climate Change-CAHOSCC) wanaokutana kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

    Alisema tatizola mabadiliko ya tabianchi linachangiwa kwa kiasi kikubwa na hewa chafu ambayo inazalishwa viwandani kutokana na matumizi makubwaya nishati.

    "Kuna vyanzo vya nishati ambavyo si rafiki na kimojawapo ni makaa ya mawe. Ili uweze kupata nishati yakeni lazima uyaunguze nakwa kufanya hivyo unatoa hewa ukaa nyingi sana. Viko viwanda vinatumia mafuta mazito, vinginedizeli kwa wingi sana. Yote haya yanachangia hewa chafuambayo inafanya utando unaozuia hewa ya joto kurudi kwenye mfumo wa sayari na kutumika tena,"alisema.

    Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari,  Waziri Mkuu alisema kiwango kikubwa cha hewa chafu inayozalishwa viwandani kutokanana matumizi ya nishati kinatoka nchi zilizoendelea wakati Bara la Afrika linazalisha asilimia tatu tu ya hewa hiyo.

    "Sisi Afrika tunapaswa tusifiwekwa kupunguza kasi ya ongezeko la jotoduniani.Nchi tajiri zinapaswa kutupongeza kwa sababu bado tuna misitu ambayo inasaidia kunyonya hiyo hewa chafu,"aliongeza.

    Waziri Mkuu alisema mkutano huo ni muhimu kwa sababu unaandaa kauli kwa ajili ya Wakuu wa Nchi watakayokwenda kuiwasilisha kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Kujadili masuala ya Tabianchi utakaofanyika New York, Marekani mwezi ujao.

    "Ninatumaini Mawaziri wote watatoka na kauli moja itayowawezesha Wakuu wa Nchi zetu waende na kauli moja. Natumaini watafanikiwa,"alisisitiza Waziri Mkuu.

    Akizungumza na washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Algeria,  Jamhuri ya Congo,  Misri, Kenya, Uganda,  Sudan,  Msumbiji, Ethiopia,  Ghana, Mauritania na wenyeji Tanzania,  Waziri Mkuu alisema suala la mabadiliko ya tabianchi yanaziathiri nchi zote duniani bila kujali kipato, umri, mahali nchi ilipo, matabakawala kazi za wananchi.

    "Nchi za Afrika ambazo kazi za uchumi wa wananchi wake zinategemea zaidi hali ya hewa, ndizo zinaathirika maradufu zikichangiwa zaidi na kukosekana kwa mbinu za kujihami pamoja na misingi dhaifu ya kiuchumi,"alisema.

    Alisema taarifa za hivi karibuni kutoka Intergovernmental Panel on ClimateChange zinaonyesha kwamba kiwango cha utoaji wa hewa chafu kila mwaka kimeongezeka kwa asilimia 2.2huku hewa chafu kutoka viwandani ikiongoza kwa kuchangia asilimia 80 ya hewa hiyo kwenye nchi zilizoendelea.

    Mapema, Kamishna wa Umoja wa Afrika anayesimamia Kilimo na Uchumi wa Vijijini, Bibi Rhoda Tumusiime alisema bara la Afrika linapaswa lijipange vizuri na kutoa matamko mazito kwenye mikutano ya kimataifa ili kukemea matumizi matumkzi makubwa ya nishati yanayochangia uharibifu wa mazingira.

    "Afrika lazima iendelee kutetea nafasi yake kwenye mikutano hii mikubwa. Lazima itoa kauli nzito kwani kuharibiwa kwa mazingira kunaathiri pia sektanyingine za utalii, maji, nishati na kadhalika,"alisema.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.