Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari, Waziri Mkuu alisema kiwango kikubwa cha hewa chafu inayozalishwa viwandani kutokanana matumizi ya nishati kinatoka nchi zilizoendelea wakati Bara la Afrika linazalisha asilimia tatu tu ya hewa hiyo.
"Sisi Afrika tunapaswa tusifiwekwa kupunguza kasi ya ongezeko la jotoduniani.Nchi tajiri zinapaswa kutupongeza kwa sababu bado tuna misitu ambayo inasaidia kunyonya hiyo hewa chafu,"aliongeza.
Waziri Mkuu alisema mkutano huo ni muhimu kwa sababu unaandaa kauli kwa ajili ya Wakuu wa Nchi watakayokwenda kuiwasilisha kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Kujadili masuala ya Tabianchi utakaofanyika New York, Marekani mwezi ujao.
"Ninatumaini Mawaziri wote watatoka na kauli moja itayowawezesha Wakuu wa Nchi zetu waende na kauli moja. Natumaini watafanikiwa,"alisisitiza Waziri Mkuu.
Akizungumza na washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Algeria, Jamhuri ya Congo, Misri, Kenya, Uganda, Sudan, Msumbiji, Ethiopia, Ghana, Mauritania na wenyeji Tanzania, Waziri Mkuu alisema suala la mabadiliko ya tabianchi yanaziathiri nchi zote duniani bila kujali kipato, umri, mahali nchi ilipo, matabakawala kazi za wananchi.
"Nchi za Afrika ambazo kazi za uchumi wa wananchi wake zinategemea zaidi hali ya hewa, ndizo zinaathirika maradufu zikichangiwa zaidi na kukosekana kwa mbinu za kujihami pamoja na misingi dhaifu ya kiuchumi,"alisema.
Alisema taarifa za hivi karibuni kutoka Intergovernmental Panel on ClimateChange zinaonyesha kwamba kiwango cha utoaji wa hewa chafu kila mwaka kimeongezeka kwa asilimia 2.2huku hewa chafu kutoka viwandani ikiongoza kwa kuchangia asilimia 80 ya hewa hiyo kwenye nchi zilizoendelea.
Mapema, Kamishna wa Umoja wa Afrika anayesimamia Kilimo na Uchumi wa Vijijini, Bibi Rhoda Tumusiime alisema bara la Afrika linapaswa lijipange vizuri na kutoa matamko mazito kwenye mikutano ya kimataifa ili kukemea matumizi matumkzi makubwa ya nishati yanayochangia uharibifu wa mazingira.
"Afrika lazima iendelee kutetea nafasi yake kwenye mikutano hii mikubwa. Lazima itoa kauli nzito kwani kuharibiwa kwa mazingira kunaathiri pia sektanyingine za utalii, maji, nishati na kadhalika,"alisema.
0 comments:
Post a Comment