Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai, mhe. Omar Mjenga, leo amemtembelea na kufanya mazungumzo na Bw. Rashid Lootah, Mwenyekiti wa Nakheel, Shirika la Nyumba la Serikali ya Dubai.
Katika mazungumzo yao, wamezungumzia ziara ya Mwenyekiti huyo pamoja na ujumbe wake kuitembelea Tanzania, itakayofanyika kuanzi tarehe 16-20 Septemba, ambako anatarajia pamoja na kuonana na baadhi viongozi wa Serikali, watafanya mazungumzo na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) yatakayowezesha kusainiwa makubaliano ya ushirikiano kwenye sekta ya nyumba kati ya mashirika hayo mawili.
Aidha, watapata fursa ya kukitembelea kituo cha uwekezaji - TIC ili kupata taarifa muhimu za uwekezaji.
Aidha, Mhe. Mjenga amemuomba Mwenyekiti huyo kufadhili mkutano wa Uwekezaji kwenye Sekta ya Utalii utakaofanyika Novemba hapa Dubai. Mkutano huo unaandaliwa na Ubalozi Mdogo kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii ya Tanzania-TTB pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Mhe. Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Lootah mbele ya baadhi ya miradi inayojengwa na Nakheel.
Mazungumzo yakiendelea kati ya Mhe. Mjenga na Mwenyekiti Lootah, katika ofisi za Nakheel.
0 comments:
Post a Comment