August 29, 2014

  • FILIKUNJOMBE: HUKUMU YA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBS EKEREGE NI NDOGO MNO


    FILIKUNJOMBE: HUKUMU YA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBS EKEREGE NI NDOGO MNO

    Na Mathias Canal, Kwanza jamii-Iringa

    Taarifa kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dsm, imemuhukumu kwenda jela miaka mitatu (03) aliyekuwa Mkurugenzi wa TBS Charles Ekerege, ni taarifa njema kwa Watanzania wote tunaojali maisha na afya zetu.
    Pamoja na kwamba hukumu iliyotolewa ni hukumu ndogo mno ukilinganisha na kosa lenyewe.Hukumu hii ni ushindi mkubwa kwa iliyokuwa Kamati Bunge ya Hesabu za Mashirikia ya Umma (POAC).Hukumu hii ni ushindi kwa Bunge. Ni ushindi kwa watanzania wote.Kwasababu pamoja na kwamba Ekelege ameshitakiwa kwa kuipotezea mapato serikali - ukweli ni kwamba sisi (POAC) tulipo kwenda kuikagua TBS tulikuta hakuna ukaguzi wowote uliokuwa ilifanyika kwa bidhaa zilikuzokuwa zinakuja Tanzania.

    Ilikuwa ni 'audit query' iliyoletwa kwetu na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
    Tukaunda Kamati ndogo ya uchunguzi.
    Tukiwa kazini, Bwn. Ekelege alifanikiwa kuidanganya Kamati ya Bunge kwamba TBS wana ofisi Hong Kong.
    Akatupeleka wabunge wa Kamati ya Bunge kwenye ofisi "feki" ya TBS. Tukambaini hadaa zake.
    Lakini pia, tukiwa Hong Kong tulikuta sticker za ukaguzi na ubora za TBS zinauzwa mitaani 'Chun King Mansion' kwa yoyote anayezitaka - hali iliyotuthibitishia zaidi kuwa hakuna chochote cha maana kilichokuwa kinafanywa na TBS, kule Hong Kong.
    Pamoja na kudai kwamba TBS wana ofisi nyingine ya ukaguzi, kule Singapore, tulipoambatana naye kwenda Singapore kwa uchunguzi, Bwn. Ekelege alishindwa kutuonyesha hata hizo ofisi zake za TBS zilipo.
    Pamoja na kwamba Mhe. Kangi Lugola ni Mlokole, bado Mhe. Kangi alipandwa na hasira; akitaka kumpiga ngumi Bwn. Ekelege, kwa udanganyifu mkubwa wa Bwn. Ekelege.
    Kangi alikuwa ni mmoja ya wabunge niliopewa na Spika kwenda kumchunguza Ekelege.
    Tukiwa kule, tulibaini kwamba Ekelege (TBS) alikuwa anaruhusu bidhaa za nje kuingia Tanzania bila ya kukaguliwa, bila kujali ubora wake.
    Tulikuta matairi feki yanaruhusiwa kuingia nchini. Tulikuta mafuta feki yanaruhusiwa kuingia nchini. Tulibaini kuwa blue band zinaingia Tz bila kukaguliwa ubora wake. Etc.
    Ni kweli huyu bwana alikuwa anatumia madaraka yake vibaya; Tulimkuta na mlolongo wa tuhuma ambazo POAC tuliziwasilisha bungeni pamoja na mapendekezo stahiki.
    Ni kwa mara ya kwanza, mwaka ule wa 2011/2012 swala la Ekelege na TBS likatuunganisha wabunge wote; Tuliweka itikadi zetu pembeni...
    Deo Filikunjombe,

    Makamu Mkiti - PAC. 


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.