August 27, 2014

  • KERO KATIKATI YA JIJI LA MBEYA: MACHINGA WAJIACHIA WAPANGA BIDHAA MPAKA BARABARANI , WAHUSIKA WAMEUCHUNA, JE MAPATO HAYA YANAENDA WAPI? NA NI SAHIHI HAWA WATU KUWA HAPA?




    KERO KATIKATI YA JIJI LA MBEYA: MACHINGA WAJIACHIA WAPANGA BIDHAA MPAKA BARABARANI , WAHUSIKA WAMEUCHUNA, JE MAPATO HAYA YANAENDA WAPI? NA NI SAHIHI HAWA WATU KUWA HAPA?
    Imekuwa ni moja ya kero kubwa na uchafuzi wa jiji katika Lango la Jiji eneo ambalo wageni , Viongozi wakubwa na watu mbalimbali wanapita.
    Kero hii ambayo wahusika mnaliona hili na mnalikalia kimya linawapa watu maswali mengi sana na mpaka kudhania labda ni kamradi kamtu na ambako hakaeleweki eleweki kuwa pato lake linaenda wapi
    Sio pengine ni kakipande tuu kutoka Eneo la Benki ya CRDB hadi Eneo la BP kona ya kuelekea Posta. Inafahamika kuwa eneo hili lilikatazwa kufanyika biashara lakini sasa imekuwa ndio eneo la watu kuweka Bidhaa zao na kila siku watu hawa wanazidi
    Je Wahusika mpo na mnalizungumziaje?
     Hapa kila mtu anaweka Bidhaa zake wenye Nguo , Viatu na vitu mbalimbali wote wapo hapa
     Kila mmoja yupo Huru tuu
     Hapa ni nje ya wakusanya mapato(TRA) wanakazana kufukuza watu wengine maeneo mengine je hawa hawawaoni? 
     Pamegeuka Duka
     Kila kitu kinapatikana eneo hili
     Hii njia ya kuelekea Posta unakaribishwa na Viatu 
     Wengine ndio kwanza wanaanza weka mzigo
     Kila mmoja anawahi kuanza biashara
     Wale Mgambo wa Jiji ina maana hapa hawakupangiwa kupita?
     Wadau hili si ni Duka kabisa!
     Je sasa hapa hawa ni Machinga ama wafanya biashara?
    Hata bei zao ukigusa hapa sio za Machinga....

    Ndugu Mdau na Msomaji wa Mbeya yetu... Toa maoni yako Juu ya Hili...

    Picha na Mbeya yetu


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.