August 14, 2014

  • KIKAO CHA MKAKATI WA UJENZI WA MAABARA ZA SHULE ZA SEKONDARI ZA KUDUMU KATA CHAFANYIKA DAR ES SALAAM



    KIKAO CHA MKAKATI WA UJENZI WA MAABARA ZA SHULE ZA SEKONDARI ZA KUDUMU KATA CHAFANYIKA DAR ES SALAAM
     Naibu Meya Manispaa ya Kinondon,Songoro Mnyonge (katikati), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), Agosti 12, 2014 jijini Dar es Salaam mara bara baada ya kufungua kikao kilichowakutanisha wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na wenyeviti wa bodi za shule chenye lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa fedha za kujenga zinajenga  maabara katika shule  za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu (kushoto), Afisa Uhusiano Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera, na kulia. Diwani Kata ya Kawe Othmani Chipeta.
     Mchumi, wa Manispaa ya Kinondoni, Bw.Salm Hamisi Msuya akielezea mchakato wa uchangiaji wa ujenzi wa maabara katika shule 18 za sekondari zilizokuwa na maabara za kudumu wakati wa kikao hicho.
     Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni, Bw.Sanga Omari akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
     Diwani kata ya Manzese, Mhe.Eliam Manumbu akichangia mada.
     Wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na wenyeviti wa bodi za shule wakiwa kwenye kikao chenye lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa fedha za kujenga maabara katika shule  za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huuHABARI PICHA- NA PHILEMON SOLOMON


    MANISPAA  ya Kinondoni inahitaji jumla ya kiasi cha Sh Bilioni 1.3 ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete aliyezitaka Halmashauri zote kuhakikisha zinajenga  maabara katika shule  za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu.

    Hayo yamebainishwa jana Jijini Dar es salaam na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Songoro Mnyonge  wakati akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na wenyeviti wa bodi za shule chenye lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa fedha hizo.

    Huku akiwaomba wadau mbalimbali yakiwemo mashirika, taasisi, watu binafsi pamoja na wafanyabiashara kujitokeza kuchangia upatikanaji wa fedha hizo, Songoro alisema ushirikiano wao katika suala hilo utaipa  faraja manispaa hiyo kutokana na umuhimu wa elimu kwa taifa.

    "Tunawaomba mjitokeze kwa wingi ili kuunga mkono juhudi za Rais Kikwete anayetaka kuona shule zote za sekondari zinakuwa na maabara za kudumu ili kusaidia kupanua wigo wa ufundishaji kw wanafunzi mashuleni, jitihada zetu pekee hazitotuwezesha kufikia malengo hayo kutokana na ufinyu wa bajeti" alisema Mnyonge.

    Aidha alisema manispaa hiyo inahitaji maabara za kudumu 114 kukidhi mahitaji katika kata 32 huku sekondari 14 ndizo pekee katika zilizo na maabara hizo kati ya 46 zilizopo katika manispaa hiyo suala alilosema linahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa haraka.

    Alisema kila chumba kimoja cha maabara ya kudumu ujenzi wake unakadiriwa kufikia kiasi cha Sh Milioni 75 na kwa jumla ya vyumba vote 114 inahitajika kiasi hicho cha zaidi ya Sh Billioni 1,suala alilosema haliwezi kufanikiwa bila nguvu za wadau mbalimbali.


    Alisema malengo ya baadae ya manispaa hiyo ni kujenga vyumba vitatu vya maabara ya fikizia, kemia na baiolojia ifikapo mwaka 2016 hatu aliyosema kwa kiasi kikubwa itamaliza tatizo la ugumu wa masomo ya sayansi kwa wanafunzi sambamba na kuongeza wataalam wa baadae wa Taifa hili.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.