August 27, 2014

  • Vodacom Tanzania yaja na Fistula Ice Bucket Challenge


    Vodacom Tanzania yaja na Fistula Ice Bucket Challenge
    Kampuni ya Vodacom Tanzania imekuja na Fistula Ice Bucket Challenge '#BongoIce' yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya akina mama wajawazito wenye ugonjwa wa Fistula. Hii ni kufuatia kampeni inayoendelea mitandaoni ikijulikana kama #ALSIceBucketChallenge ambapo Vodacom Tanzania kwa kutambua kuwa kuna wanawake wengi Zaidi ya 30,000 wanaogua ugonjwa huu hapa nchini imeanzisha kampeni inayoitwa #BongoIce.

    Mkurugenzi wa Vodacom, Rene Meza amekuwa wa kwanza kushiriki kampeni hii na kuwateua Naibu Waziri wa Mawasiliano Mhe January Makamba, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Tigo Diego Gutierrez na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airtel ndugu Sunil Colaso kushiriki kampeni hii. Fuatilia kupitia:


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.