Hii ni Barabara inayo anzia Sae kuelekea Mwambene, Wakazi wa eneo hili wanazingatia usafi
Hakuna Chembe ya takataka Mitaro kila kitu kipo sawa
Usalama wa Barabarani umewekwa sawa kabisa kuna matuta ambayo hayawezi sababisha Gari likagonga chini hata kama likiwa fupi
Haya ni Maeneo ya Mwambene
Hapa ni eneo mojawapo eneo la Mwambene ambapo Barabara hii ilikuwa ni korofi sana, sio kipindi cha masika wala cha ukame palikuwa hapapitiki lakini kwa sasa mambo safi kabisa inapitika vizuri.
Ingawa Barabara imefika mpaka Mwambene kuna umuhimu wa hivi vibanda upande wa kushoto vikaondolewa na kuweka Maduka ambayo yatapendezesha mji.. Jiji hapo vipi?
Hii ni Njia ya kuelekea Ilomba ukitokea Mwambene
Moja ya Kona kali ambayo inatokea Ilomba kuelekea Mwambene
Haya maeneo ya Ilomba
Njia za wapita kwa miguu nazo zimeboreshwa
Shughuli mbalimbali zikiwa zinaendelea
Hapa ni Makutano ya barabara inayoelekea Mwambene, Sae, Block Q na Ilomba
Bajaji zikiwa zimekaa katika mpangilio tayari kwa safari eneo la Mwambene
Endelea kufuatilia Tochi yetu ya Mbeya yetu uone tutamulikia mitaa ipi
PICHA NA MBEYA YETU
0 comments:
Post a Comment