Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt, Rehema Nchimbi akitoa ufafanuzi kuhusu makabidhiano ya Rasimu ya katiba yatakayofanywa kati ya viongozi wa Bunge maalumu la katiba watakao kabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Jakaya Kikwete na wa Zanzibar Dkt Mohamed Sheni kwa waandishi wa habari, makabidhiano hayo yatafanyika Oktoba 08, 2014 katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.(Picha na John Banda wa Pamoja Blog)
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt, Rehema Nchimbi kwa makini wakati alipokua akielezea kuhusu makabidhiano ya Rasimu ya katiba yatakayofanywa keshokutwa Oktoba, 08 mwaka huu katika uwanja wa jamhuri ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete na Dkt Mohamed Sheni ndiyo watakabidhiwa.
WANANCHI wa mkoa wa Dodoma na mikoa jirani wametakiwa kufika katika uwanja wa jamhuri mjini Dodoma jumatano ya oktoba 8, 2014 kwa ajili ya kushuhudia tukio la kihistoria kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr. Ally Mohamed Shein kukabidhiwa katiba iliyopendekezwa na bunge maalumu la katiba.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema Tukio hilo litafanyika hapa mjini Dodoma kwenye viwanja vya Jamhuri kuanzia saa 6:00 Mchana na Milango ya uwanja wa Jamhuri itafunguliwa kuanzia saa 12:00 asubuhi.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema watu watakaojitokeza ili kushuhudia tukio hilo watakuwa wengi hivyo kwa kuzingatia kuwa milango ya uwanja wa Jamhuri itafunguliwa mapema, wananchi wanashauriwa kuwahi kufika viwanja vya Jamhuri na kuhakikisha kuwa kila mtu atakayehudhuria awe tayari amekaa kwenye nafasi yake ifikapo saa 5:00 asubuhi.Dkt Nchimbi amesema tukio hilo litahudhuriwa na Marais wastaafu wa Tanzania, Marais wastaafu Zanzibar, Viongozi wa kitaifa na watendaji wakuu, Viongozi wakuu wastaafu, Maspika wastaafu, Waheshimiwa Mabalozi na wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa, Taasisi za Kidini, Taasisi zisizo za kiserikali na wamiliki wakuu wa vyombo vya habari.
Amesema Vilevile kutakuwepo na Makundi mbalimbali kutoka mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar. Makundi hayo ni pamoja na Wafugaji, Wakulima, Wavuvi, Wanawake, Vijana, Wazee, Wachimbaji madini wadogo, Walemavu na Wasanii.
Aidha Dkt, Nchimbi ameseama Tukio hilo la Kihistoria litatanguliwa na tukio muhimu na maalum la kuomba Dua na Shukrani kwa kukamilika salama kwa shughuli za "Bunge Maalum la Katiba" hapa Mkoani Dodoma tofauti na nchi nyingine katika viwanja vya Nyerere Squere hapo kesho saa 10 jioni.
0 comments:
Post a Comment