October 24, 2014

  • YOUTH FOR AFRICA (YOA) YATAMBULISHA TUZO ZA VIJANA CHINI MIAKA 30



    YOUTH FOR AFRICA (YOA) YATAMBULISHA TUZO ZA VIJANA CHINI MIAKA 30
    Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Youth For Africa (YOA) Harisson Anthony Mbugi ( wa pili kulia) akiongea na wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutambulisha rasmi tuzo za vijana chini ya miaka 30. Kushoto kwake ni Meneja mauzo na masoko wa Push Mobile, Ezekiel Mukundi akifuatiwa na Ofisa YOA, Abdul Lukanza. Utambulisho uliofanyika Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam Oktoba 2-2014.

    Youth For Africa (YOA), Shirika la kitaifa linaloongozwa na vijana ambalo makao yake yapo Dar es Salaam linapenda kuwataarifu wanahabari na umma kuhusu tuzo za vijana chini ya miaka 30 kwa mwaka 2014 ( Under-30 youth Awards 2014). 

    Tuzo hizi ni kubwa na za kwanza za aina yake zinazowalenga vijana moja kwa moja. Tuzo za mwaka huu zinakuja na ujumbe 'Zaidi ya Kawaida' ikiwa ni katika kuwapa moyo na kuwahamasisha vijana kufanya vitu vizuri zaidi katika maendeleo yao binafsi, jamii na nchi kwa ujumla.

     Tuzo hizi za vijana wenye umri chini ya miaka 30 zinalenga kutambua vijana wa kitanzania walio chini ya miaka 30 ambao wamefanya vizuri katika nyanja mbalimbali na kuwatia hamasa wao na vijana wote wazidi kuwa na ndoto, wazidi kujifunza na wazidi kufanya vitu vizuri zaidi katika nchi.

    Youth For Africa (YOA) pia inapenda kuwataarifu wanahabari na umma kwa ujumla kuwa upendekezaji wa majina ya vijana wanaostahili hizi tuzo (kuanzia miaka 18 hadi 29) ushafunguliwa na unazingatia vipengele 15 vilivyopo tuzo hizi.

    Vipengele hivyo ni pamoja na Kilimo, Uvumbuzi, Mchango kwa Jamii, Ubunifu Mitindo, Uanamitindo, Muziki, Uigizaji, Ujasiriamali, Wazo zuri la Biashara, Michezo, Utangazaji, Tovuti bora, Uchapishaji, Sanaa, Uanataaluma..

    Tunapenda kuwatambua na kuwashukuru wadhamini wetu waliojitokeza mpaka sasa ambao ni pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Uongozi Institute, Push mobile, Africa Media Group Ltd [Channel 10 & Magic fm], FastJet , Onspot Magazine, Smartcodes ,Kalax Promotions and Adam Digicom. Tunapenda kuchukua nafasi hii pia kuwakaribisha wadau mbalimbali waweze kudhamini tuzo hizi ili kuweza kutimiza malengo ya tuzo hizi.

    Upendekezaji wa majina utaendelea mpaka tarehe 10 Novemba 2014. Mapendekezo yanatumwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu au kupitia tovuti yetu. www.youthawards.com.

    Kupitia ujumbe wa simu (maelezo jinsi ya kushiriki):
    Tuma neno " Under30 " kwenda 15678 upate kujua vipengele vyote na code zake. Ukishakujua kodi za kila kipengele andika ujumbe mfupi wenye kodi ya kipengele unachotaka kupendekeza mtu ikifuatiwa na jina la mtu unayempendekeza na namba yake ya simu au barua pepe kasha utume kwenda 15678.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.