Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiweka Jiwe la Msingi kuashiria ujenzi wa njia za kupitishia wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiwahutubia wananchi waliofika katika Hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mh. Norman Sigalla akitoa neno la Shukurani
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Seif Mhina akitoa Taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Mwenyekiti wa Kamati ya Marafiki Olise Ole Seenga akisoma Taarifa fupi juu ya ujenzi huo wa barabara za kupitishia Wagonjwa katika Hospitali ya Mkoa
Mshehereshaji Mwakilili akiendelea kutoa Mwongozo
Kaimu Meneja wa Kanda nyanda za Juu Kusini NMB Joel Uswege ambao pia ni Marafiki wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya akitoa neno
Meneja masoko wa Masoko wa AJ Technology Mbeya Eliah Susuwe ambao pia ni Marafiki wa Hospitali ya Rufaa Mbeya akitoa neno wakati wa sherehe hizo
Mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata huduma katika Hospitali ya Mkoa akiongea na Mkuu wa Mkoa kueleza jinsi huduma Bora zinazotolewa na wauguzi wa Hospitali ya Mkoa.
Katikati ni Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkoa Mbeya Glory Mbwile
Hii ni moja ya njia hizo
Hii ni Sehemu ya Mita 104 ambazo bado hazijakamilika
Picha ya Pamoja
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka wananchi kuunga mkono juhudi ya Kamati ya Marafiki wa Hospitali ya Mkoa walioamua kujenga njia za kupitishia wagonjwa zenye urefu wa mita 411.
Wito ameutoa katika Hospitali ya Mkoa alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi ambao umefadhiliwa na Kamati ya marafiki waliojitolea kujenga njia hizo kutokana na adha kubwa wanayopata wagonjwa wanaofika katika Hospitali hiyo kupata huduma mbalimbali za matibabu.
Akisoma risala kwa Mkuu wa Mkoa Mwenyekiti wa Kamati ya marafiki Olise Ole Seenga amesema kuwa mpaka hivi sasa wamebakiwa na mita 146 ambazo hazijaguswa kabisa kutokana na ukosefu wa pesa jumla ya shilingi milioni 150 ili kukamilisha ujenzi huo.
Aidha Seenga amesema kuwa mita 104 zimesakafiwa kwa saruji lakini hazijaezekwa kabisa hivyo kuwaomba wananchi wajitokeze ili kukamilisha ujenzi huo ulioanza mapema mwezi Mei mwaka huu baada ya kufanyika Harambee ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa ambapo jumla ya shilingi milioni 80 zilipatikana.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro aliipongeza kamati ya marafiki,Waandishi wa habari na wadau waliochangia fedha na mali kwa moyo wa uzalendo waliouonesha hata kufanikisha kuanza kwa ujenzi huo.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa alipokewa kwa furaha na wagonjwa waliokuja kupata huduma katika hospitali ya Mkoa kutokana na utaratibu mzuri walioupanga ambao hautoi upendeleo kwa wagonjwa na kuipongeza hospitali kwa utaratibu wa elimu kwa wagonjwa kabla ya matibabu.
Kandoro alihitimisha ziara yake kwa kuutaka uongozi wa Hospitali kuboresha mandhali ya hospitali ili iwe faraja kwa wagonjwa wanaokuja kupata huduma na ametoa woto kwa watu walioahidi kuchangia ujenzi huo kwa kushindwa kufanya hivyo wanajidhalilisha utu wao na pia wanakwamisha juhudi kwa kuwa tamko lao liliingizwa kwenye makisio.
Na Mbeya yetu Blog
0 comments:
Post a Comment