October 14, 2014

  • WAZIRI NYARANDU ATOA SOMO KWA TANAPA


    WAZIRI NYARANDU ATOA SOMO KWA TANAPA
    Waziri wa Maliasili na utalii, Lazaro Nyarandu, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika mkutano wake uliofanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

    Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakimsikiliza waziri




    HIFADHI za taifa Tanzania (TANAPA) imetakiwa kuainisha maeneo yote yenye vivutio vya utalii ambayo yanawezekekana kuendelezwa na kuyatangaza kwa wananchi wote ili kila mwenye uwezo wa kuwekeza apewe nafasi.

    Hayo yalibainishwa na Waziri wa Maliasili na utalii, Lazaro Nyarandu, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika mkutano wake uliofanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika mapumziko mafupi wakati akielekea mkoani Njombe kumuwakilisha Waziri Mkuu.

    Nyarandu alisema Serikali inamikakati ya kuhakikisha Watanzania ndiyo wanapewa vipaumbele vya kuwekeza katika sekta za utalii kwa kujenga nyumba za kulala watalii, kujenga makambi, kujenga na kuendeleza vivutio pamoja na kutembeza watalii.

    Alisema jambo hilo litasaidia kuinua sekta ya utalii nchini ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha watanzania kutembelea hifadi mbali mbali na sio kusubiri wageni kutoka nje ya nchi.

    Alisema ili kuongeza kasi ya watalii kuingia nchini kila mwananchi anapaswa kujifunza kukarimu wageni hususani wahudumu wa mahoteli ambao wamekuwa wakiwahudumia wageni kila wakati ili wawe na moyo wa kurudi tena.

    Kwa upande wa ujangili na mauaji ya Tembo Waziri Nyarandu alisema hivi sasa kuna mafanikio makubwa kutoka na kila Mwananchi kushiriki kulinda hifadhi na kuzuia majangili kuua wanyama ovyo kama ilivyokuwa awali.

    Alisema hivi sasa kuna ongezeko kubwa la Tembo tofauti na kipindi cha nyuma baada ya serikali yake kuweka mikakati kabambe ya kuwakabili wawindaji wote ikiwa ni pamoja na kuwafungia leseni wawindaji waliokuwa wakiwinda kinyume cha sheria na kuhusika kwenye mauaji ya Tembo.

    Aliongeza kuwa hata mfumo wa kukabiliana na ujenzi holela wa makazi na mahoteli ndani ya hifadhi za wanyama umechangia kuongezeka kwa uzalishaji wa Tembo ambapo alisema kwa takwimu za mwaka jana kuna ongezeko la tembo zaidi ya 70,000.

    Alisema hivi sasa Serikali haina idadi kamili ya tembo walipo nchini katika mbuga zote ambapo imeshaingia makubaliano na nchi wahisani ili kufanya sense ya Tembo na Faru ili Serikali iwe na idadi halisi ya wanyama hao nchini.

    Alisema kazi hiyo imeshaanza kufanyika ambapo Mwisho wa mwaka huu wanatarajia kupata majibu ambayo Serikali itawangazia wananchi wote ili wajue idadi ya Tembo na Faru waliopo katika kila hifadhi na mbuga za wanyama nchini.

    " Hivi sasa kusema ukweli kabisa mimi Waziri hata nikiulizwa swali leo kuwa tuna tembo wangapi nchini sina majibu kwa sababu hakuna mtu anayejua na wala hatujawahi kuhesabu jambo tunalitarajia kulifanya sasa" alisema Waziri.

    Mwisho.

    Na Mbeya yetu



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.