
Lori aina ya Scania namba T              607 CWV Semi Taller (kama linavyoonekana katika picha)              lililokuwa limebeba kokoto limeanguka katikati ya lami muda              huu katika eneo la Chalinze Mzee Mkoani Pwani na kuharibika              vibaya.
                      
Kwa mujibu wa Mashuhuda,                ajali hiyo ametokea baada ya gari hilo lililokuwa                likielekea Dar es Salaam, kuteleza kutokana na mvua                iliyonyesha asubuhi ya leo mkoani humo.
            
Hata hivyo askari wa                usalama barabarani wamefika eneo la tukio na kufanikiwa                kuliondoa gari hilo ambalo limesababisha foleni kubwa ya                magari yaliyokuwa yakitokea jijini Dar es Salaam kwenda                mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha kutokana na kuziba                barabara.
           
0 comments:
Post a Comment