October 30, 2014

  • TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI



    TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
    DSC00217
    MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA YASSINI HEZRON (14) MKAZI WA KIWIRA ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.235 AFB AINA YA M/CANTER LILILOKUWA LIMEBEBA MATOFALI LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE FREDY MPONDO KUSHINDWA KUPANDA MLIMA NA KISHA KURUDI NYUMA NA KUANGUSHA MATOFALI NA KUSABABISHA KIFO KWA TINGO HUYO.
    AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 29.10.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO MAENEO YA NEW LAND BAR, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA TUKUYU/KYELA. CHANZO CHA AJALI NI GARI HILO KUSHINDWA KUPANDA MLIMA NA KURUDI NYUMA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE WA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
    TAARIFA ZA MISAKO:
    JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. OTHAZ ANGOLILE (18) 2. SAMSON MWANGOMILE (46) 3. FORD SAMSON (20) NA 4. BARAKA JOSEPH (23) WOTE WAKAZI WA AIRPORT JIJINI MBEYA WAKIWA NA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA BOSS NA RIDDER PAKETI 108.
    WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 29.10.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA AIRPORT, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. WATUHUMIWA NI WAUZAJI WA POMBE HIZO NA TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA/KUUZA POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
    Imesainiwa na:
    [AHMED Z. MSANGI – SACP]
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.