Huu ni mtaa wa kanisa, mtaa maarufu sana ambao upo maeneo ya Sokomatola Jijini Mbeya , Mtaa huu ambao upo sawa na mitaa mengine ya Jirani ambayo kwa hakika yote ina Lami tena ya kupendeza. lakini mtaa huu pekee wa kanisa hauna Lami na barabara yake ni korofi sana, baadala yake sasa inatumika sana kwa ajili ya kupitishia mifugo aina ya Punda.
Wakazi wa Mtaa huu wa Kanisa pia kwa nyakati tofauti wamekuwa wakilalamika sana kwamba hakuna anaye tikisika hata kukwangua na kuwa kero kubwa sana wakati wa kiangazi kwa kuwa na vumbi la kutosha na wakati wa masika kwa kuwa na tope la kutosha .
Twende pamoja ushuhudie mtaa huu wa Kanisa Njia Kuu ya Mnyama Punda wa kubeba mizigo
Kwa makini Muongozaji wa Punda hao ambaye kwa hakika jina lake halikupatikana kwa mara moja akiwa anawavusha wanyama hao kwa makini
Sasa Punda hao wanaingia katika Mtaa wao wa Kujinafasi Mtaa wa Kanisa
Wale wanaenda zao , wakati huo huo endelea kutazama jinsi Barabara hii ambavyo imesahaulika
Picha halisi ya Mtaa wa Kanisa ambapo barabara yake ni ya vumbi huku mitaa mengine yote imetandazwa Lami
Bara Bara ilivyo Korofi
Hakuna unafuu katika Barabara hii, wananchi wanaamua kutupa taka hovyo bila kujali
Mabonde ya kutosha
Ukitazama vizuri hapo utaona mtaa wa Kanisa ulivyo chafuka kwa Ubovu na kwa mbele utaona Lami , sasa je hapa katika mtaa wa huu Jiji walikuwa hawana Ramani kupaweka sawa?
Hakuna Mvua hapa lakini tazama kwa makini watu wanavyo tembea kwa adabu katika mtaa huu maana ukitembea vibaya kwa mguu waweza jikwaa na kudondoka kabisa
Huu ndio Mtaa wa Kanisa
Mtaa unaofuatika Mara baada ya huu wa kanisa ni Lami tupu
Mtaa huu Mwengine nao ni Lami tupu
Hata huu nao ni lami Tupu..
Sasa Tunauliza Huu mtaa wa Kanisa umekosa nini?... Jibu unalo mdau karibu kwa maoni yako, pia kama kuna mnaoishi mtaa huu mtuambie inakuwaje nyie hamtengenezewi Barabara yenu hata kwa kukwetulia acha maoni yako hapa chini.
PATA SETI HII IFUATAYO KWA TSH 67,000 TUU NI SETI YA FORONYA 4, SHUKA KUBWA , NA KAVA MOJA NZITO YA KUFUNIKIA BLANKETI NA VITU KIBAO. NI RAHISI PIGA SIMU NAMBA 0654221465 AU 0683167574
0 comments:
Post a Comment