………………………………………………………….
Na Saidi Mkabakuli
Serikali imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka wa fedha 206/2017 ili kuongeza kasi ya kufikia lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo imedhamiria kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini kufikia mwaka 2025.
Akizungumza wakati wa kuwakaribisha Ugeni kutoka Tume ya Mipango na Maendeleo ya China, Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Kiuchumi, Bw. Paul Sangawe, amesema kuwa Tanzania imedhamiria kuaandaa Mpango wa miaka mitano utakaojikita katika uchumi wa viwanda ndani ya muda mfupi ujao.
"Tumedhamiria kuwekeza nguvu zetu kwenye uwekezaji katika viwanda; katika Mpango wa Pili wa Maendeleo, nguvu kubwa tunaiweka katika maendeleo ya viwanda ili kuweza kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025," alisema Bw. Sangawe.
Akizungumza wakati wa kikao cha pamoja na viongozi wa Tume ya Mipango ya Tanzania, Kiongozi wa Msafara huo, Bw. Wang Jianjun ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye fursa kubwa ya kufikia maendeleo na kuweza kuondoka kwenye kundi la nchi maskini ndani ya kipindi kifupi kijacho.
Bw. Jianjun aliongeza "ili kuweza kufikia maendeleo ya haraka zaidi, ni vyema Tanzania ikaanza kuwekeza katika viwanda hasa kwenye Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZs) ili kuongeza tija katika uzalishaji na kuongeza thamani bidhaa zake ili kuvutia masoko toka nje ya nchi.

0 comments:
Post a Comment